Meneja wa wasanii ambaye pia ni kiongozi wa kituo cha Mkubwa na wanawe Mkubwa Fella, amesema yeye hana tofauti na msanii yeyote, na kudai anaweza kufanya kazi hata na Alikiba ambaye wengi wanadhani ana tofauti naye kubwa.
Mkubwa Fella ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio, na kusema kuwa hajawahi kugombana na Alikiba na anaweza kufanya naye kazi, kwani Kiba ni mwanaye wa dhahabu.
"Mimi kwanza sijawahi kusema sifanyi kazi na mtu yeyote, kwanza Alikiba mimi mwanangu wa dhahabu, mwanangu wa gold wala usiseme kuna kitu hichi, mimi ndiyo meneja wa kwanza katika mziki huu sina pingamizi ya kusema nitafanya kazi na mtu au niogope kufanya kazi na mtu, wote wanangu mimi ni mkubwa na wanawe, Alikiba mwanangu haijawahi kuonekana hata siku moja mimi na Alikiba tunagombana, sijakuwa hivyo", alisema Mkubwa Fella.
Kwa muda mrefu kumekuwa na dhana kuwa Mkubwa Fella hawezi kufanya kazi na msanii Alikiba kwa kuwa meneja huyo amekuwa karibu sana na watu kutoka WCB ambao wanaonekana kuwa tofauti na Alikiba, lakini leo Mkubwa Fella amezima hizo dhana na kusema yeye anaweza kufanya kazi na Alikiba
No comments:
Post a Comment