Kampuni
ya simu ya Tecno Mobile iliyoingia makubaliano ya kibiashara na Timu maarufu
inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu
nchini Uingereza Klabu ya Manchester City, kwa pamoja wamekuja na mikakati ya
kukuza soka nchini Tanzania.
Kwa
Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na
Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Bwana
Eric Mkomoye, amesema kua pamoja na kuwapo kwa fursa za kibiashara zilizopo
kati ya klabu ya Manchester City na Tecno Mobile lakin pia Tecno wamedhamiria
kutumia fursa hiyo kukuza viwango vya mpira kwa watoto wa kitanzania ambao
wazazi wao pia ni wateja wa kampuni hiyo
Katika
ushirikiano huu pia imeleta simu maalumu itakayotumika alama maalumu ya
Tecno Mobile na klabu ya Manchester
City, Eric alifafanua.
“Tumeleta Tecno
Camon CX Manchester city limited version, ni simu maalumu inayoonesha
ushirikiano wetu na Man city pia ni simu
maalumu inayotumika wachezaji wa Manchester city katika kupiga
picha , hivyo tumeileta sokoni maalumu kwa wateja wetu kipindi waweze
kupata experience wanayopata man city
katika simu hii.”
Aliongeza
“Simu hii inakuja na box kubwa lenye zawadi maalumu kwa wateja kama chupa ya
kimichezo, speaker, fimbo maalumu ya kupigia picha pamoja na kava maalumu.”
TECNO
Mobile wameleta simu ikiwa ni toleo maalumu la tecno camon cx iliyokua sokoni
mapema kidogo ila limeboreshwa Zaidi, hivyo inaenda na wakati uwezo wa kamera
yake ni 16mp nyuma na mbele zinazosaidiwa na flashi mbili mbele na nne nyuma,
uwezo wake ndani ni 64 GB huku ikisukuma data vizuri kwa 4GB Ram,
No comments:
Post a Comment