Wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao na
kujenga tabia ya kuzungumza nao kuwashirikisha kwenye mambo mbalimbali hususani
afya ya uzazi ili kuwalinda na kuwasaidia kupambana na changamoto zinazowakabiri
wawapo majumbani na waendapo mashuleni na sehemu nyingine.
Hayo yamesemwa jana na washiriki wa Semina za GDSS
zinazofanyika kila jumaa tano zinazoandaliwa na Mtandao wa Jinsia TGNP, lengo
likiwa ni kuwakutanisha wakazi mbalimbali wa kata za jiji la Dar es salaam
kujadili changamoto zinazowazunguka ndani ya jamii yao na namna ya kuzitatua.
Na jumaa tano hii mada ilikuwa ni kujadili “Changamoto
mbalimbali wanazokutana nazo watoto wa kike kwenye idara ya elimu”.
Baadhi ya washiriki wa Semina GDSS wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji wa Semina hiyo Bi. Agness Lukanga akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema jana jijini Dar es salaam |
Kwa mujibu wa washiriki wa semina imeonekana kuwa changamoto
kubwa ni Uchumi hii inatokea pale mzazi anaposhindwa kumtimizia mahitaji muhimu
mtoto wake, hivyo mtoto inamlazimu kuyatafuta kwa njia nyingine ambayo ni mbaya kama kuwa
nawanaume waliomzidi umri hali inayosababisha kupata mimba au kuambukizwa
Magonjwa ya zinaa kama Ukimwi.
Lakini pia Malezi mabaya yanachangia kumuharibu mtoto na kwa
hali ya sasa ambayo kila mzazi anakuwa yuko bize na mambo yake ya kutafuta pesa
bila kujari mtoto kama anaenda shule na pia kufuatilia nyendo na maendeleo ya
mtoto wake, hivyo walio wengi hushtuka mtoto akiwa tayari ameshaharibika uenda
kapata mimba au kawa na tabia zisizokubalika kwenye jamii.
Bi. Tatu Kitenge akitoa hoja yake kwenye semina ya GDSS iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia(TGNP) mapema jana jijini Dar es salaam |
Utandawazi pia ni changamoto kubwa kwani wanafunzi wa sasa
wanamiliki simu kubwa(smart phone) na wazazi wanashindwa hata kuwahoji watoto
wao kama hizo simu wanazitoa wapi? Lakini pia wanafunzi hao hao hutumia simu
hizo hizo kuangalia picha za ngono na kuangalia vitu vingi vya kutoka nje
ambavyo ni tofauti na maadili yetu wa afrika.
Kushindwa kuenzi Mila na Desturi za zamani pia ni tatizo kwa
watoto wa sasa kwa kuwa zamani ulikuwa ukikosea mtu yeyote mkubwa anakukanya
ikiwezekana kuchapwa, lakini kwa sasa hata ukimkuta mtoto wa jirani yako
anafanya mambo yasiyofaa ukijaribu kumkanya kwa kumchapa, mama yake anakuja juu
na inawezekana hata ukapelekwa kituo cha polisi na ukamlipa pesa kwa kosa la
kumpiga mtoto hali inayowapa watoto wa sasa kiburi.
Bw. Oscar Raphael akitoa maoni yake kwenye Semina iliyofanyika mapema jana kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Dar es salaam |
Lakini pia Sharia zimekuwa zikiwapa kiburi watoto hasa
wakike ukimpiga anaweza kukufungulia kesi mahakamani na ukafungwa kutokana na nasheria
zinazomlinda mtoto. Lakini huenda ulikuwa na lengo zuri kwa huyo binti la
kutaka asipotee kimaadili, au pia ulimkuta sehemu isiyostahili kwa muda huo
labda muda wa darasani yeye kaka kijiweni na wahuni, au yupo kwenye kichochoro
na baba aliyemzidi umri kwa lengo la kumrubuni lakini ukimuadhibu sharia inakufunga kwa kosa
la kumpiga mtoto.
Vishawishi vya ngono ni miongoni mwa sababu inayokwamisha
watoto wa kike kupata elimu hasa kwa wale wanaosoma shule za mbali, wanashawishiwa na makondakta pamoja na madereva wa dala dala pamoja na madereva
wa boda boda kwa kuwapa lifti au fedha wanafunzi hao na baadae kuwataka kimapenzi.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Umoja Jesca Saimoni akitoa maoni yake kwenye Semina ya GDSS iliyofanyika mapema jana kwenye ukumbi wa Mtandao wa Jinsia(TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam |
Lakini pia mashuleni kuna baadhi ya walimu ambao sio waaminifu
wanawataka wanafunzi kwa kuwatishia kuwapa adhabu au kuwapa matokeo mabaya
kwenye mitihani yao hali inawafanya wanafunzi waoga kukubali na matokeo yake
kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba au virusi vya Ukimwi.
Ugomvi mpaka kufikia kutengana kwa wazazi hii inamuweka
kwenye nafasi mbaya mtoto wa kike, pale anapokenda na mama yake na baadae baba wa
kambo anamtaka binti huyo kimapenzi, au kupelekwa kwa ndugu kama mjomba na baba
mdogo na hatimaye binti huyo kunyanyaswa au kufikia kubakwa na hao hao ndugu
zake.
No comments:
Post a Comment