WATOTO watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Karatu na kwenda kutibiwa nchini Marekani, watawasili kesho asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Arusha.
Watoto hao ambao ni Doreen, Sadia na Wilson waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani tayari wameshapanda ndege kutoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kupata nafuu.
Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.
Shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea na kuchangia chochote kusaidia matibabu ya watoto hao.
No comments:
Post a Comment