Mkutano wa nane wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza kesho mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa ofisi ya Bunge ratiba ya bunge itatolewa leo baada ya kamati ya uongozi kukutana na kuamua uwasilishwaji wa mswada iliyopo
Katika mkutano huo wabunge wa chama cha Cuf wanatarajiwa kuapishwa kutokana na baadhi ya wabunge kufukuzwa baada ya kukikuka utaratibu na miongozo ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kutohudhuria vikao.
Juzi mbunge mmoja ambaye alitarajiwa kuapishwa na wenzake kesho Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda alifariki dunia na kuzikwa jana makaburi ya Kisutu.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha
Hindu alifariki dunia ghafla nyumbani kwake Kibada Kigamboni.
Sakaya amesema Hindu alikuwa ni mpambanaji na mtu mwenye kukijenga chama hicho kuanzia miaka ya 90 hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.
‘’Hata ukifika Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.
“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.
No comments:
Post a Comment