MSANII mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli ambaye hivi karibuni amekuwa akitamba na wimbo wake wa Orugambo baada ya kurudi kwenye game ya muziki, mkali huyo leo September 4, 2017 ameliamsha dude kwa kuachia video mpya ya wimbo wake ‘Kichaka’.
Katika wimbo huyo, Saida mwenye sauti ya kipekee, amewashirikisha G Nako wa Weusi na Belle 9 ambao kwa pamoja wameutendea haki wimbo huo.
Ngoma hiyo ambayo imeshutiwa hapa hapa Bongo, imeaandaliwa na Director Hanscana.
No comments:
Post a Comment