Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Humphrey Polepole siku ya leo tarehe 8 mwezi wa 9 ameungana na Mtandao wa jinsia TGNP katika kuhitimisha Tamasha la Jinsia kwa mwaka huu 2017.
Polepole ameshiriki vizuri katika Tamasha hilo kwa kutembelea mabanda na miradi mbalimbali iliyopo katika tamasha hilo, pia wageni waalikwa wamepata nafasi ya kubadilishana mawazo, kupiga picha na kucheza muziki na kiongozi huyo.
Akiongea na Habari 24 blog Mh. Polepole amezungumzia nafasi ya wanawawake katika ukuzaji uchumi, lakini pia usawa wa kijinsia katika chama cha mapinduzi(CCM) na malengo yaliyowekwa katika chama hicho ili kukuza uchumi wa wanawake.
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ZAIDI..
No comments:
Post a Comment