Wananchi pamoja na waandishi wa habari waliopata nafasi
ya kuhudhuria katika Tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017, wametakiwa kuwa na
utamaduni wa kuhoji juu ya mipango na maazimio yanayowekwa baada ya kukamilika
kwa tamasha hilo.
Mwenekiti wa bodi ya TGNP Mtandao Bi. Vicensia Shule akiongea na waandishi wa habari mapema jijini Dar es salaam |
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mtandao Bi. Vicensia Shule
alisema kuwa leo tunahitimisha tamasha letu lililodumu kwa muda wa siku 4
kuanzia tarehe 5 mpka 8 ya mwezi septemba, hivyo basi wadau pamoja na waandishi
wa habari muwe na utamduni wa kuwa mnatuhoji kuhusiana na kile tulichokipanga kama
kweli tumeweza kukitimiza.
Miongoni mwa
mipango hiyo ni kuhakikisha kuwa TGNP mtandao wanatafuta taarifa na kuzifanyia
uchambuzi yakinifu ili kutoa takwimu sahihi kuhusu mimba na ndoa za utotoni,
ukatili wa kijinsia na umiliki wa ardhi kwa wanawake na watu wenye ulemavu.
Na mpango
wapili ni kuendelea na utamaduni wake wa
kutambua na kuenzi michango ya wanawake mbalimbali waliofanya vizuri katika
kuleta maendeleo kwa ngazi jamii, taifa na kimataifa.
Lakini pia kutoa
mafunzo ya kuchukua na kutunza kumbukumbu za wanawake hao na kuzisambaza kwa azaki,
vijana na wadau mbalimbali ili waweze kujifunza kupitia wao lakini pia kuweza
kurithi kati ya kizazi kimoja na kingine.
Bi vicensia
aliendelea kwa kusema wataweka mipango endelevu ya kurithi ujuzi na maarifa kwa
wanawake waliobobea katika tasnia mbalimbali kwa vizazi na lika moja kwenda
lingine.
Alisema kuwa baadhi
ya wanawake walioleta mabadiliko ya kweli na kuweza kutunukiwa tuzo ni kama Mheshimwa
Samia Suluhu,Getrude Mongella,Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Anne Makinda,Profesa Daktari Esther Mwaikambo,Anna Abdallah na Esther
Bulaya.
Wengine ni
wanachama wa TGNP Mtandao waliotoa mchango mkubwa katika kujenga Tapo la
Ukombozi wa wanawake kimapinduzi akiwemo Profesa Marjorie Mbilinyi,Asseny
Muro,Mary Rusimbi,Demere Kitunga,Subira Kibiga,Aggripina Mosha na Zippora
Shekilango.
Waandishi wa habari wakiendelea kuchukua matukio katika mkutano wa viongozi wa TGNP Mtandao na waandishi wa habari mapema jijini Dar es salaam. |
Na bila
kuwasahau vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania kuweza kushiriki katika Nyanja zote kuhakikisha
rasilimali za kutosha zinatengwa kuhakikisha utekelezaji wa mipango na mikakati
ya vijana inatekelezeka bila kuangalia itikadi, jinsi, dini, jografia na hali
ya kimapato.
No comments:
Post a Comment