Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetakiwa kuweka sharia madhubuti za kuwaadhibu
watu wanaondeleza vitendo vya ukeketaji kwa wanawake kote nchini.
Hayo yamesemwa
mapema leo katika warsha iliyoandaliwa na Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu
yenye lengo la kupinga ukeketaji na kutokomeza kabisa vitendo vya ukeketaji kwa
wanawake na wasichana.
Akiongea na
waandishi wa habari kiongozi mkuu wa timu ya watafiti Dr. Geofrey Chambua alisema
kuwa wao utafi wao umelenga zaidi kwa wanawake wenye umri wa miaka 18 na
kuendelea kwani kundi hilo ni kama limewekwa pembezoni.
Alisema kuwa
utafiti huo umefanywa katika mikoa mitatu ambayo ni vinara kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa na Tume ya Taifa ya Utafiti ambayo imeonyesha kuwa mkoa wa Manyara
unaongoza kwa kuwa na 58% Mara 32% na Singida 31.
Aliendelea
kusema kusema kuwa kundi la umri wa miaka 15 – 19 ni asilimia 5 peke yake na
kundi lililobaki la kuanzia miaka 20 na kuendelea ni lenye tatizo kubwa zaidi,
na wao wanahisi ni kutokana na kuwa sharia inawalinda watoto hao na hao wengine
hakuna sharia inayowalinda.
Lakini jambo
lingine ni wananchi kuwa waoga wa kutoa taarifa endapo wanatendewa vitendi hivi
lakini pia wazazi au walezi wanaogopa kutengwa na familia au jamii kwa kutoa
ripoti polisi kwa kuwa ni utamaduni wao.
Na lingine
kwa hawa wenye umri wa miaka 20 na kuendelea ni watu wazima wanaojitambua
lakini pia ukubali kukeketwa kwa sababu ya kupata fursa sawa na wengine kwani
mwanamke asiye keketwa utengwa na jamii nzima na pia kukosa mume kwa kuonekana
kuwa hajakamilika.
Aidha dr.
chambua alipenda kushauri vyombo husika vya maamuzi kama bunge kutunga sharia zinazolinda
makundi yote na siyo kuangali kundi la mabinti wenye umri mdogo peke yake kwani
kitendo cha kumfanyia ukeketaji mwanamke ni kumkosesha haki yake kimsingi.
Lakini pia
kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na yanayohusika na haki za mwanamke na mtoto
pamoja na jamii kwa ujumla kuungana kwa pamoja kusambaza elimu hii kuondoa
tatizo la ukeketaji.
Bila kusahau
kundi muhimu la Viongozi wa dini zote na madhehebu yote kuweza kushirikiana kwa
pamoja kutoa elimu hii kwa waumini ili waache kukeketa kwa kujua siyo jambo
zuri la kufanyiwa mwanamke wa umri wa wowote.
No comments:
Post a Comment