Kampuni ya TECNO imeonesha ni kwa jinsi gani inathamini
wateja wake kwa kuaandalia hafla maalumu
kuwapongeza wateja wa simu mpya ya
TECNO SPARK.
Mkuu wa mauzo kwa Upande wa TECNO mkoani Mwanza akiwa tayar kukabidhhi zawadi kwa mshindi. |
TECNO inayofanya kampeni ya simu mpya iliyopatia umaarufu mkubwa nchini TECNO SPARK imewaandalia wateja wake hafla ya maalumu ya kuwashukuru kwa kuwaunga mkono pamoja na kuwapa zawadi za aina mbalimbali ikiwemo simu mpya ya TECNO SPARK iliyokwenda kwa mshinid bwana Baraka Modo mkazi wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Afisa Mahusiano wa TECNO bwana , Eric
Mkomoye amesema kwamba TECNO inaendeleza utaratibu wake wa kuwajali wateja wake
kupitia matukio mbalimbali yatakayokua
yanaandaliwa kwa nia ya kuwapongeza wateja wa TECNO na kuwaweka karibu na
kampuni hiyo kama ambavyo mteja wao katika hafla hiyo bwana Baraka Modo alivyojishindia TECNO SPARK.
Mshindi wa SPARK Bwana, Baraka Modo akikabidhiwa zawadi yake na timu ya mauzo ya TECNO mkoani Mwanza. |
Wateja wa Tecno mkoani Mwanza walipata nafasi ya kuingia kwenye hafla hiyo
maalumu iliyoitwa TECNO BLUENIGHT baada ya kununua simu ya TECNO SPARK, huku
wengine wakipata tiketi kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO.
TECNO inaendelea kuwahimiza wateja wake kujumuika
katika kampeni mbalimbali inazoziendesha ili
wateja waweze kufaidika zaidi.
Timu ya TECNO ikiwa tayari kwa hafla maalumu jijini Mwanza. |
Simu iliyowezesha wateja hao kuwepo katika hafla
hiyo maalumu ni TECNO SPARK simu mpya iliyojipatia umaarufu mkubwa nchini kwa
umbo lake la kuvutia, ikiwa ina usalama wa alama za vidole (finger print), kioo
chake ni kikubwa huku ikiwa na camera ya 13mp nyuma na 16gb za kuweka data za
aina zote katika simu bila kutumia kadi kumbukumbu (Memory kadi).
No comments:
Post a Comment