Mambo muhimu matano yanayotakiwa katika kumuwezesha mwanamke
wa kiafrika ambayo hawayapati mabinti waliopata mimba mashuleni na hii ni ndani
ya familia au jamii iliyowazunguka.
Mwanachama wa TGNP Mtandao Bi. Rehema Mateba akiongoza Warsha ya kupinga ukatili dhidi ya wanafunzi waliopata mimba mashuleni katika Tamasha la 14 la Jinsia Mabibo Dar es salaam. |
Akiongoza warsha hiyo ya kupinga ukatili dhidi ya watoto waliopata mimba shuleni Bi. Rehema Mwateba alisema kuwa mambo haya ni muhimu sio tu kwa mabinti waliopata mimba mashuleni bali ni kwa kila binadamu, ila kwa watoto hawa imekuwa kama ni desturi kutopewa kwa kuonekana wao ni wakosaji zaidi watu wote.
Miongoni
mwa mambo hayo ni yafuatayo.
1. Ustawi – ni ile hali ya kukua vyema kwa kupata
mahitaji yale muhimu ya kibindamu ambayo akiyakosa mtu yoyote basi hakuna maisha,
na hii inajumuisha mahitaji yanayopimika na yale yasiyo pimika mfano wa
mahitaji yanayopimika ni vitu kama Chakula,
Mavazi, Malazi pamoja na Maji, na mahitaji yasiyopimika kama Upendo, Furaha, Heshima,
Kusikilizwa, Kuthaminiwa kupatiwa Ulinzi, kuchangamana na wengine nk. Kwaiyo
unakuta hivi vyote wanavikosa wasichana waliopata mimba mashuleni.
2. Ufikiaji rasilimali – hii pia ni changamoto
kubwa wanayokutana nayo wasichana wanaopata mimba mashuleni kwani kutokana na
kutopewa heshima nyumbani au hata katika jamii hali inayowafanya wawe na msongo
wa mwazo na kushindwa hata kuzitumia vizuri rasilimali walizo karibu nazo kama
Zahanati inaweza kuwa karibu lakini ikashindwa kumnufaisha binti huyu.
3. Kupata Muamko – hii ni ile hali ya kushtuka na
kuchukua hatua ya haraka endapo umedhamilia kufanya jambo Fulani, lakini kwa
wasichana hawa wanashindwa kupata miamko kwa kuwa bado akili hazijapevuka na
kujijua kuwa sasa nina mimba inabidi nifanyaje kuhusiana na hili? Na pia wanashindwa
kuchukua hatua ya haraka, lakini pia kujua kuwa nahitajika niende kwa wataalamu
wa uzazi ili wanisaidie kwa mabinti hawa wanakuwa hawana fikra hizo na mpaka
akipata muamko inakuwa ni siku ya kujifungua .
Diwani wa Mwadui Luhombo mkoani Shinyanga Mh. Sarah Masinga akitoa ufafafanuzi wa jambo fulani katika Tamasha la jinsia la 14 lililoandaliwa na mtandao wa jinsia TGNP. |
4. Kushiriki na kushirikishwa – hii ni ile hali ya
kuwepo na kupewa nafasi ya kusikiliza na kutoa maoni yako katika kitu chochote
cha kifamilia hata cha kijamii pia. Lakini kwa wazazi wengi hawaliangalii hili
wakiona binti yao kapata ujauzito hawampi nafasi ya kumsikiliza katika maamuzi
ya hali ya afya yake lakini pia hata kumshirikisha katika mambo ya kifamilia
kwa kumuona kama ni mkosefu.
5. Kumiliki mali – hili pia ni tatizo kubwa sana
sio tu kwa wahanga wa mimba za mashuleni bali ni kwa wanawake wengi wanakumbana
nalo tatizo hili la kutomilikishwa mali.
Na kwa upande wa wahanga wa mimba za mashuleni kwa familia nyingi hawapewi
kabisa nafasi hizi kwani wanaonekana kuwa wameshakuwa wakubwa ndio maana
wamepata mimba, hivyo wazazi wengi
uamini kuwa binti huyo atamiliki mali ya mumewe ambae ndio aliyempa mimba hiyo.
Muwezeshaji wa TGNP Mtandao Mama Rehema Mateba akiendelea kutoa elimu kwa vijana, wazazi toka mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kupinga ukatili unaofanywa kwa mabinti wanaopata mimba shuleni. |
Hivyo basi kutokana na hali hii wanageni
toka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara
na Visiwani walipendekeza mapendekezo yafuatayo .
Kwanza kutoa elimu kwa wazazi ili waachane
na mila potofu kwamba binti akipata mimba shuleni basi nafasi yake ya kusoma
imeishia hapo, lakini pia watambue kuwa hata kama kapta mimba akiwa shuleni
bado ni mtoto wao na anatakiwa kupewa mahitaji kama mtoto mwingine na suruhisho
sio kumfukuza au kumpiga.
Lakini pia jambo lingine ni kutumia marafiki
wa elimu waliyoenea karibu mikoa yote ya Tanzania bara kwani wao wanatoa misaada
ya kimawazo na kujua watakupa mbinu gani ili mtoto aendelee na elimu, lakini
pia kumpa darasa litakalomuongoza kufikia malengo yake kwani kupata mimba sio
mwisho wa maisha ya shule.
No comments:
Post a Comment