Zanzibar. Makamu
wa Rais, Samia Hassan Suluhu amezindua rasmi leo Jumatano shughuli za Kamisheni
ya Kiswahili Afrika Mashariki, lengo
ikiwa ni kuisogeza karibu taasisi hiyo muhimu ya lugha kwa nchi
wanachama.
Pia, Mama
Samia alizindua mpango mpango mkakati wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika
Mashariki ukiwa na lengo la kuhimiza matumizi ya lugha hiyo kwa nchi wanachama katika
nyanja mbalimbali.
Alisema
kamisheni hiyo imekuwa ikifanya kazi zake kwa takribani miezi sita lakini awali ilikuwa haijazinduliwa jambo ililofanya
watu wengi kutofahamu shughuli zake.
Akuzungumza
kwenye kongamano hilo la kimataifa la kwanza linalofanyika Zanzibar kwa siku tatu,
Mama Samia alisema ili kushirikiana kwenye nyanja tofauti umoja wa forodha,
soko la pamoja, sarafu moja na ushirikiano wa kisiasa lugha ya Kiswahili inatakiwa kuenziwa kwa sababu ndicho
kiunganishi.
Pia aliwaomba
nchi wanachama wa kamisheni hiyo kuongeza juhudi kwenye mtumizi ya Kiswahili kwani
wasijionye wanyonge kuliko wengine huku akisema serikali za nchi wanachama
zitakuwa zikichangia bajeti ya kamisheni hiyo.
Aidha, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Balozi Augustine Mahiga
aliwataka wananchi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kukitumia
Kiswahili kutokana na kuwaunganisha watu wote.
Alisema
licha ya kuwepo kamisheni lakini imekuwa ni fursa ndani ya jumuiya kutokana na
baadhi ya wanachama ambao hawafahamu vyema lugha za Kiswahili kuomba walimu wa
Kiswahili kutoka Tanzania.
Kongamano
hilo linashirikisha nchi zaidi ya saba ambazo ni Rwanda, Burundi, Kenya,
Uganda, Sudan Kusini, DR Congo na wenyeji Tanzania huku wageni wengine wakitoka
kwenye mataifa rafiki kama vile Namibia na Msumbiji.
No comments:
Post a Comment