Wanaharakati
wametakiwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano(TEHAMA) katika
kuleta ukombozi na kupinga vitendo ukatili wa kijinsia.
Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika semina ilifanyika mapema jana TGNP Mtandao. |
Hayo
yamesemwa jana na afisa habari wa
mtandao wa jinsia nchini TGNP Bi. Monica John alipokuwa akiendesha semina ya
wanaharakati wa jinsia na maendeleo GDSS, yenye lengo la kujadili changamoto
mbalimbali zinazotokea wakati wa kuripoti/ kuufahamisha uma habari za ukatili
wa kijinsia.
Kupitia
semina hiyo imeonekana kuwa watu wengi hawatumii mtandao kama sehemu ya
kupashana habari na matokeo yake inakuwa ni sehemu ya kuwadhalilisha na
kuwafedhehesha wanawake, kwani kuna wanaume wengi wakiachana na wanawake zao
uweka picha za utupu za wapenzi wao mtandaoni na picha hizo usambaa mpaka
ufikia wanawake hao kudhalilika katika jamii na wengine ufikia hatua ya kujiua
ili kuondokana na aibu hiyo.
Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John akiandika baadhi ya mapendekezo ya wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo GDSS. |
Lakini pia
tatizo lingine ni kwamba vyombo vingi vipo kwa ajili ya maslahi hivyo wamiliki wanahitaji
kuona story zinazouza kama ni kwenye magazeti au kuangaliwa sana kwa upande wa
television na haswa zile stori pendwa za watu mashuhuli kama Diamond, Tundu Lissu,
mgogoro wa CUF nk. Ndizo wamiliki wanahitaji kuziona kwenye vyombo vyao na sio
kuangalia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vingine vinavyomyima
haki mwanamke na mtoto.
Bi. Subira Kibiga akitoa maoni yake katika semina za jinsia na maendeleo GDSS jana makao makuu ya mtandao wa jinsia TGNP, |
Aidha
ilionekena kuwa sehemu za vijijini ni miongoni mwa maeneo ambayo wanawake
hukosa nafasi ya kuzijua fursa na kupata habari kwani njia za kupata habari kwa
maeneo hayo ni simu na radio, wakati kwa upande wa simu mtandao unakuwa
unasumbua hivyo inalazimika kupanda juu ya mti au mlima ili kuwasiliana na kwa
upande wa radio inakuwa shida kutokana kwamba nyenzo hiyo uwa anakuwa nayo baba
muda wote akinda shambani au akienda kwenye pombe anatembea nayo hivyo kwa mama
aliye nyumbani anashindwa kufahamu mambo mengi yanayoendelea duniani.
Na jambo
lingine ni kwa upande wa wanawake ambao wamepata fursa ya kupaza sauti au kupata vipindi kwenye radio hawavitumii vizuri
katika kuwaelimisha wanawake wenzao namna ya kuzipata fursa na matokeo yake
hutumia kuwasanifu na kuwaongelea vibaya wanawake hao, na waliowengi wenye muda
kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana mfano wa vipindi kama Leo Tena cha Gea
Habibu na Dina Marios wakina Bibi Hindu na Lady Hanifa wa Radio One nk.
Bw. Innocent Siliyo akichangia mada katika semina za GDSS mapema jana makao makuu ya mtandao wa jinsia TGNP Mabibo Dar es salaam. |
Baada ya
majadiliano yote waliazimia mambo kadhaa kupitia semina hiyo kuu likiwa
wanawake kwa pamoja kuunda chombo chao cha habari ili kuweza kupaza sauti zao,
kwani tatizo limeshaeleweka kuwa vyombo vingi vilivyopo vinaangalia biashara na
siyo ukombozi wa wanawake na watoto ili kuleta usawa wa kijinsia.
Na azimio la
pili ni serikali kuweka sharia nzuri zinazowalinda wanawake mitandaoni kwani
inaonekana mwanamke kudhalilishwa mtandaoni ni jambo la kwawida au pengine yeye
mwenyewe anapenda hali hiyo, lakini pia watumiaji wa mitandao wametakiwa
kukemea hali hiyo endapo wanaiyona kwa mwanamke kusambaziwa picha zake akiwa
hana nguo kitu ambacho sio kizuri kwa jamii yetu na kuacha kuendelea kusambaza
kwa wengine.
Baadhi ya washiriki wa semina za jinsia na maendeleo wakifuatilia kwa umakini mada iliyoongozwa na Monica John ambae ni Afisa habari wa TGNP Mtandao. |
Kwa waandishi
pamoja na wahariri kupenda kuripoti habari za ukatili wa kijinsia kwani
wananchi wanahitaji kufahamu mambo mengi kuhusiana na vitendo hivyo, na kujua
endapo watafanyiwa wanatakiwa kuchukua hatua zipi ili waweze kushinda swala la
ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment