Kituo cha sheria na haki za Binadamu lhrc kimeviomba vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu.
Ombi hilo limetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dkt Hellen Kijo Bisimba wakati akitoa tamko la maadhimsho ya siku ya amani duniani.
Dkt hellen amesema endapo vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu nchini vitafumbiwa macho vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Aidha Bi Kijo amewataka wananchi kutambua kwamba wao ndio walinzi wa kwanza wa amani nchini hivyo wanapaswa kufuata sheria na kuepuka vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo Mapema leo |
Katika kuadhimisha siku hiyo Kituo Hicho kilijipanga kufanya maandamano ya amani kuahamasisha amani Nchini lakini kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi hellen Kijo Bisimba,Jeshi la polisi liliwanyima Kibali cha kufanya hivyo kwa kile kilichoitwa kuwa na Viashiria vya uvunjifu wa amani
Kauli mbiu ya siku amani duniani kwa mwaka 2017 ni “pamoja kwa ajili ya amani, nidhamu, usalama na heshima kwa wote”
No comments:
Post a Comment