Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani.
Wanajeshi hayo ni;
- Hamad Haji Bakari,
- Chazil Khatibu Nandonde,
- Idd Abdallah Ally,
- Juma Mossi Ally,
- Ally Haji Ussi,
- Pascal Singo,
- Samwel Chenga,
- Deogratius Kamili,
- Mwichumu Vuai Mohamed,
- Hassan Makame,
- Issa Mussa Juma,
- Hamad Mzee Kamna,
- Salehe Mahembano na
- Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.
Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani
No comments:
Post a Comment