Thursday, December 14, 2017

Serikali yapiga marufuku filamu zinazoamasisha ushoga...soma habari kamili na matukio360..#share


WAZIRI wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amepiga marufuku uoneshwaji wa filamu  zenye kuhamasisha ushoga nchini.
Dk. Harrison Mwakyembe.
Ametoa agizo hilo  leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Mwakyembe amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaodai kuwa kuna filamu za kiphilipino zinazohamasisha ushoga.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko ya kuwepo kwa filamu za kiphilipino zinazohamasisha ushoga, leo nina kikao na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kujadili hilo,” amesema.

Dk. Mwakyembe amesema ikiwa watathibitisha malalamiko kuwa ya kweli, miongoni mwa hatua serikali itakayochukua ni kuzuia uingizwaji na uoneshwaji wa filamu hizo kwani ni kinyume na utamaduni wetu.

 Ameleza kuwa moja ya sababu za kuingizwa kwa filamu hizo nchini ni kutokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuziruhusu baada ya kulipiwa kodi bila kushirikisha vyombo vya udhibiti wa ubora wa filamu nchini ambavyo ni kosota na bodi ya filamu.


Ameongeza kuwa tamko rasmi dhidi ya uingizwaji na uoneshwaji wa filamo za namna hiyo nchini litatolewa baada ya kikao hicho baina yake na TCRA.

No comments: