Afisa habari wa shirika la Utu wa Mtoto(CDF) Michael Sungusia akitoa mchango wake katika semina ya kuwajengea uwezo wanahabari ili kuweza kuripoti habari za kulinda na kutetea haki za mtoto. |
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa umakini semina iliyoandaliwa na shirika la Utu wa Mtoto(CDF) mapema leo jijini Dar es salaam. |
Muwezeshaji wa semina ya kuwajengea uwezo wanahabari kuweza kuripoti habari za kulinda na kutetea haki za watoto Bi. Edna Kamaleki akiongea na wana habari mapema leo jijini Dar es salaam. |
NA MUANDISHI WETU
Waandishi wa habari wametakiwa kuwa makini waandikapo habari za kuhusu watoto, hii ikiwa ni pamoja na kufuata misingi na sharia ya mtoto.
Hayo yamesemwa
mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Lecri Consult ambaye
pia ni mshauri wa maswala ya haki za watoto Bi. Edna Kamaleki alipokuwa
akiongoza semina kwa wanahabari kuhusu uvunjwaji wa haki za mtoto na namna ya
kuzilinda haki hizo.
Bi Edna
amesema kuwa vema wanahabari wanapotaka kutoa taarifa yeyote inayomuhusu mtoto kuzingatia
maadili ya uandishi wa habari lakini pia sharia zinazomlinda mtoto huyo.
Sharia imeweka
wazi kuwa mtoto aruhusiwi kupigwa picha au kurekodiwa pasipokuwa na ridhaa yake
au mzazi/mlezi wake na pia hairuhusiwi kutumia sauti yake, jina kamili wakati
akielezea au kufanya kitu chochote kitakacho mtambulisha yeye ni nani.
Mkurugenzi huyo
aliendelea kusema kuwa sharia inamuhesabia makosa kwa mtu yoyote aliyeshuhudia
au anajua kuwa kuna mtoto amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili na hakuchukua
hatua yeyote kama kutoa taarifa mahali husika, mtu huyo anapigwa faini ya shilingi
50 elfu au kifungo jela au mda mwingine vyote viwili.
Baada ya
kusema hayo Bi. Edna alipenda kuwashauri watunga sera na viongozi walio katika ngazi ya maamuzi kujaribu kurekebisha
baadhi ya sharia zinazokinzana pamoja na kurekebisha sharia zinazolalamikiwa
kuwa zimepitwa na wakati na zinazowanyonya watoto hasa wa kike.
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ZAIDI..
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ZAIDI..
No comments:
Post a Comment