HABARI MPYA

POLISI WADAI NABII TITO ANAMATATIZO YA AKILI SOMA HAPA KUJUA

Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito.

JESHI la Polisi mkoani Dodoma,  baada ya kumkamata na kumfanyia mahojiano Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito, kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya, limesema mtu huyo ana  matatizo ya akili.

Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gillesi Muroto, amesema mnamo Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.