Thursday, January 25, 2018

SABABU TATU ZA SUGU KUMKATAA HAKIMU MTEITE KUSIMAMIA KESI YAKE.

HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite hii leo ametoa uamuzi wa kutojitoa na kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.  Pia mawakili watatu wa utetezi wamejitoa katika kesi hiyo.
Hatua hiyo inafuatia baada ya Sugu na mwenzake Emanuel Masonga  ambaye ni katibu mkuu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini kumkataa hakimu huyo.Wanakabiliwa na kesi ya uchochezi na wamerudishwa rumande hadi Februari 8, 2018.

Hata hivyo mbunge Sugu ameomba wiki mbili za kupanga kujitetea

Sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Sugu na mwenzake ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuria mahakamani hapo mara kwa mara ili hali Hakimu anataka kesi hiyo iishe mapema.

SABABU TATU ALIZOTOA SUGU KUMKATAA  HAKIMU

“Mheshimiwa Hakimu dhamira yangu imenituma nikukatae wewe Hakimu, kwa sababu tatu zifuatazo…

1. Sijawahi kuona hakimu yuko bias kama wewe ikiwemo kuninyima dhamana bila sababu za msingi kisheria na kikatiba.

2. Jana nilishuhudia kielelezo cha tape recoder kikitoka mikononi mwa Mwanasheria wa serikali kuja mahakamani kinyume cha sheria na hoja za wakili wangu Mwabukusi ulizipinga.

3. Kwenye mabishano umekiri kesi hii imekupa shida, mi ni Mkristo sitaki upate shida naomba nikukatae ili aje hakimu mwingine aendeshe kesi kwa uhuru bila kupata shida na mazingira ya shinikizo lolote lile.

Kwa sababu hizo naomba nikukatae and  I’m very serious about it, nakukataa”

No comments: