Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
Na Bashir Nkoromo, Pugu
Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.
Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo, Waziri wa Mifugo na Uvivi Luhaga Mpina ametoa agizo hilo kunusuru hali ya fukuto la mapigano katika ya wafanyabiashara kwenye mnada huo kudai Wanakijiji hicho cha Bangulo kuvamia eneo la malisho.
"Baadhi yenu mmeonyesha hapa hati za kumiliki makazi, lakini pia tunafahamu kuwa eneo la Mnada lilikuwa na ukubwa wa ekari 190, hivi sasa limebaki eneo kama asilimia 20 tu ya malisho. Hali hii inaufanya Mnada huu kukosa sifa, hivyo wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu naagiza shughuli zote za ujenzi na kilimo zisimame kwanza kuanzia leo," alisema Mpina.
Waziri Mpina amewataka wananchi kuishi bila hofu akisema suala lao litapatiwa ufumbuzi ambao utakuwa wa kudumu.
Habari katika Picha
Sehemu ya eneo la Mnada wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkaribisha kufanya ziara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alipowasili kwenye Mnada wa Pugu wilayani hummo, Dar es Salaam, leo
Waziri Mpina akimsalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipowasili kwenye Mnada wa Pugu leo
Waziri Mpina akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kabla ya kuanza ziara
Sohia Mjema akimuongoza Waziri Mpina kwenye eneo la kufanya mazungumzo na uongozi wa Mnada huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo
Mkuu wa Mnada wa Pugu Kevamba Samwel akizungumzia hali ya maendeleo na changamoto za Mnada huo
Matibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na mkuu wa Mnada huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akieleza anavyozijua na alivoanza kuzishughulia baadhi ya changamoto za Mnada huo hasa mgogoro wa arhi baina ya Mnada na Wananchi
"Naona mda unakwenda mbio, hebu tuanze utembeleaji mipaka..." akasema waziri Mpina huku akitazama saa yake
Waziri Mpina akijadiliana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kipi waanze kati ya kuzungumza kwanza na wananchi au kukagua mipaka
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akiwa ameweka bakora begani wakati safari ya kukagua mipaka ikianza. Kushoto ni Katubu wa Mwenezi tawi la CCM Bangulo Kata ya Pugu Stesheni Loyce Hamisi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kushoto) akiongoza kupanda moja ya vilima vilivyo katika Kijiji cha Bangulo wakati akikagua mipaka ya kijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema naye akijiandaa kupanda kilima hicho
"Kwa hiyo hadi kulee ni eneo la malisho ya Mnada?" Waziri Mpina akiuliza maofisa aliofuatana nao. Wapili kushoto ni DC Mjema
Afisa wa Mnada akimpatia maelezo waziri Mpina kuhusu lilivyo eneo la malisho ya Mnada wa Pugu
Kamanda wa Polisi wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi Salim Hamduni akiongoza msafara wakati wa kushuka baada ya Waziri Mpina kukagua badhi ya maeneo ya mipaka kati ya kijiji cha Bangulo na Mnada wa Pugu
Kisha waziri Mpina naye akashuka kilima hicho
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Bangilo kinachodaiwa kuvamia eneo la malisho ya Mnada wa Pugu. Kushoto ni Waziri Mpina
"Wenyewe mpo?" Waziri Mpina akiuliza huku akichungulia kwenye geti la nyumba moja inayoonyesha kujengwa hivi karibuni ambayo inadaiwa kuwa miongoni mwa nyumba za wananchi wa kijiji cha Bangulo waliovamia eneo la malisho la Mnada wa Pugu.
Aloyce Malya mkazi wa Kijiji cha Bangulo akizungumza wakati waziri Mpina alipozungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya wanankijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
Kisha Aloyce akatia hati yake ya umiliki wa ardhi na kumkabidhi waziri Mpina
Waziri Mpina akiipitia kwa makini hati hiyo baada ya kuipokea
Hati yenyewe kwa karibu
Waziri Mpina akizungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mipaka kati ya wananchi na Mnada wa Pugu
Wananchi wakimsikiliza waziri Mpina
Waziri Mpina akiwaaga baada ya mazungumzo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Wednesday, February 28, 2018
PICHA - ANGALIA WALICHOKIFANYA ACT WAZALENDO MKOANI SHINYANGA
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho mkoani Shinyanga jana kwenye kikao cha ndani . |
MJADALA WA KITAIFA UNAHITAJIKA KUHUSU FAIDA ZA MATUMIZI YA MBEGU ZA GMO KATIKA KILIMO
Mwenyekiti wa Kavazi la kwanza la Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2018 Dkt. Ng’wanza Kamata ambaye ni mahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), akichokoza mada kuhusu matumizi ya mbegu za GMO na teknolojia ya uhandisi jeni katika kilimo. Kulia ni Dk.Richard Mbunda kutoka UDSM.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dar es Salaam jana.
Mkutano ukiendelea.
Dk.Richard Mbunda kutoka UDSM, akielezea changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi ya mbegu za GMO katika kilimo.
Usikivu katika mkutano huo.
Dkt. Aloyce Kulaya akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Dkt. Adolphine Kateka akichangia.
Dkt. Goodluck Ole Medeye, akielezea umuhimu wa mbegu hizo katika kilimo.
Alfred Mmbaga kutoka Tanzania Meat Board akichangia mada.
Elisa Greebe kutoka Chuo Kikuu cha Leeds akichangia.
Mkulima mdogo Ernest Likoko akichangia mada.
Dk Emmarold Mneney akichangia mada kwenye mkutano huo.
Emma Nyerere kutoka Taasisi ya Pawo Pan African Women Organisation Tanzania akichangia jambo.
Dkt. Nicholous Nyange, akizungumza kwenye mkutano huo.Mada zikichangiwa. |
Dkt.Roshan Abdallah kutoka Agricultural Innovation Research Foundation Tanzania, akichangia jambo.
Na Mwandishi Wetu
WASHIRIKI wa Kavazi la kwanza la Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2018 wameomba elimu zaidi itolewe kwa jamii ili kusaidia kuwa na uelewa wa pamoja kama nchi katika kuelekea kutumia teknolojia ya uhandisi jeni kukablina na changamoto zinazomkabili mkulima nchini kwa sasa na kuinua tija.
Wakichangia mjadala huo uliolenga kuangalia nafasi ya mbegu za GMO na teknolojia ya uhandisi jeni katika kilimo wadau hao kutoka sekta na taasisi mbalimbali nchini wamesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na watafiti kwa kushirikiana na serikali na makampuni mengine ya nje jamii inahitaji kuelimishwa ili kuondokana na mashaka ambayo yamekuwa yakizunguzwa na baadhi ya wadau kuhusu mbegu hizo.
Wamesema wakulima wengi uzalishaji wao ni mdogo kutokana na kutumia zana duni,kutozingatia kanuni bora za kilimo,Mbegu zisiszo bora na teknolojia zingine ambazo zimewafanya wakulima kuendelea kubaki palepale na kuona kilimo sio kazi yenye tija na thamani kama kazi zingine na hivyo wadau hao kuomba mjadala mpana ufanyike wa kitaifa kuhusu teknolojia ya GMO na kuona kama ina mchango katika kusaidia kumkomboa mkulima kutoka katika hali yake ya sasa.
Akizungumzia umuhimu wa mbegu hizo za GMO kwa taifa na wakulima nchini aliyekuwa (Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika serikali ya awamu ya nne) ????? Dkt. Goodluck Ole Medeye alisema kuwa mchakato wa kuanza au kutokuanza kutumia mbegu za GMO ulianza zamani lakini serikali kupitia waalamu wake walikaa chini na kutathimini uhitaji wa teknolojia hiyo na kuona kuwa ni mkubwa na hivyo kuamua kuwapa nafasi watafiti kufanya kwanza utafiti ili kujiridhisha juu ya faida na hasara zake.
Alisema kuwa yeye binafsi alikuwa mtu wa kwanza kupinga matumizi ya mbegu zinazotokana na teknolojia hiyo lakini baada ya kuwapa nafasi watafiti kueleza na kuwaelimisha mawaziri na viongozi wengine wa serikali aliona kuwa hakuwa sahihi na kwa pamoja wakafikia uamuzi wa kuwaruhusu watafiti wafanye utafiti nchini ili kujiridhisha kuwa na uwezo wa kutambua mbegu na bidhaa zitokanazo na teknolojia hiyo.
Dkt. Medeye aliongeza kuwa hakuna namna ambayo Tanzania itakwepa kutumia mbegu hizo au bidhaa za GMO kwakuwa Tanzania sio kisiwa kama nchi zinazoizunguka Tanzania zinafanya tafiti kwa kasi na kutumia mbegu hizo basi Tanzania itajikuta wananchi wake wanatumia mbegu hizo kwani kwa sasa nguo nyingi tunazovaa zinatoka nchi zinazozalisha pamba ya GMO na baadhi ya vyakula tunavyokula kutoka nje vinatokana na mbegu za GMO.
Waziri huyo wa zamani amebainisha kuwa wakulima wengi wa Tanzania kwa miaka nenda rudi bado wanazalisha chakula kidogo sana ambacho hakikidhi mahitaji ya kaya zao na kupata ziada kwaajili ya kuuza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo zana dunia,kutotumia mbinu bora za kilimo na hasa mbegu bora hivyo ni wakati sasa nchi ikaona umuhimu wa kumuinua mkulima kwa kumpatia mbegu zenye kumletea matumani na tija.
Kwa upande wake mtafiti mstaaafu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dkt. Nicholous Nyange ambaye alikuwa mtafiti kwenye masuala ya tafiti za bioteknolojia za kilimo nchini aliyewasiliasha mada juu umuhimu wa teknolojia na mbegu za GMO amesema kuwa inakadiriwa kuwa Tanzania kwa sasa inawatu wapatao milioni 58 na idadi hii inaongezeka kila siku na kama sayansi haitatumika kusaidia kuzalisha chakula cha kutosha basi huenda taifa likasumbuliwa na njaa kila mwaka kwenye maeneo mengi.
Alisema wakulima pamoja na jitihada kubwa zinaofanywa na wakulima kulima na kupanua mashamba kila siku lakini bado hawajaweza kuzalisha chakula cha kutosha kutokana nasababu mbalimbali ikiwemo wadudu,magonjwa na changamoto zingine zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Ukame kwenye maeneo mengi ya nchi kwa sasa.
Dkt,Nyange amesema kawimu zinaonyesha kuwa Tanzania kwenye uzalishaji wa mahindi unakadiriwa kufikia ati ya tani 1.5 hadi tani mbili pale ambapo hali ya hewa na mtawanyiko wa mvua utakuwa mzuri lakini kwa nchi zilizoendelea kama vile marekani wanazalisha tani 8 hadi 9 kwa ekari kutokana na kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji .
Alisema kuwa pamoja na uchumi wa taifa kukua kwa silimia 7 lakini kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa mtanzania ambao zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanakitegemea chenyewe kinakua kwa asilimia 3 tu na hivyo kusema kuwa kama teknolojia ikitumika na wakulima wakawezeshwa kilimo kitaweza kuchangia vyema kwenye pato la taifa na kuwanufaisha wakulima ambao tunaona TASAF inawapa fedha kupitia mpango wa serikali wa kusaidia kaya masikini.
Aliongeza kuwa eneo linalofaa kwa kilimo na makazi likigawanywa kwa idadi ya watu waliopo nchini katika kipindi kifupi kichacho halitatosha kupata maeneo ya kutosha kwaajili ya kilimo makazi na shughuli zingine za kibinadamu hivyo njia pekee ni kuwawezesha wanananchi na wakulima kutumia mbinu za kisasa kuzalisha kwa wingi kwenye maeneo madogo ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu na eneo la nchi lililopo ambalo haliongezeki.
Kwa upande wake Dkt. Aloyce Kulaya mtafiti wa zao la mahindi mstaafu na mshauri wa mradi wa Water efficient Maize for Africa (WEMA) alisema kuwa suala la GMO linaangalia tuu kwenye vyakula lakini teknolojia hiyo inatumika zaidi kwenye kutengeneza madawa kama yale ya kisukari na kubainisha kuwa hata kama dawa ya ukimwi ikipatikana basi inaweza kuwa kwa kutumia njia hii pekee na sio nyingine.
Alisema teknolojia ya uhandisi jeni sio ndio njia pekee ya kupata ufumbuzi wa matatizo ya wakulima lakini pale mbinu za kawaida zinaposhindwa ndio teknolojia hiyo pekee hutumika katika kupata ufumbuzi wa haraka na sahihi wa changamoto za magonjwa,ukame na wadudu ambazo zinawasumbua wakulima nchi nzima ambayo binu za kawaida zimeshindwa.
Dkt. Kulaya aliongeza kuwa kwa wasiwasi wa watu kuwa mbegu za asili zitapotea hauna maana kwakuwa mbinu hizo za kuupatia mmea kinga na uwezo wa kuwa na sifa fulani kunaweza kufanyika pia kwenye mbegu zetu za asili na hivyo kuziwezesha mbegu hizo kuhimili magonjwa,wadudu na changamoto zingine na kumuwezesha mkulima kupata mazao ya kutosha.
Kwa upande wake Profesa, Rwaitama ameitaka serikali kuwezesha vituo vyetu vya utaifa nchini kuwa na uwezo wa kufanya tafiti hizi ambazo zinaweza kusaidia kuwainua wakulima kupambana na changamoto zinazowakabili badala ya kutegemea wafadhili pekee ambao wanapoleta fedha kwenye utafiti Fulani wanakuwa na vigezo vyao na sio lazima view kipaumbele cha nchi.
Alisema vituo vingi vya utafiti vya zamani vilikuwa vinafanya kazi nzuri katika kazi za utafiti lakini kwa sasa vimeshuka utendaji wake na kuonekana kuwa na mchango mdogo sana kwa maendeleo ya nchi ili kuweza kuwa na udhibiti wa kile kinachozalishwa kuwa mali ya taifa kwakuwa kitakuwa kimezalishwa kwa kutumia fedha za wananchi.
Prof. Rwaitama akitolea mfano wa utafiti wa Panya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) alisema ni moja ya matunda makubwa ambayo yanaipatia Tanzania na watafiti wake heshima kubwa katika kutumia panya kufanya kazi mbalimbali kubwa duniani kama vile kutambua mabomu,makohozi ya TB kwa haraka.
Naye Mwenyekiti wa mkutano huo Dkt. Ng’wanza Kamata ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) alisema kuwa Kavazi la Mwalimu Nyerere litaendelea kufanya mijadala juu ya jambo hili kila mara ili kusaidia kuwepo kwa mjadala mpana katika kujadili faida na hasara za teknolojia ya Uhandisi jeni kabla teknolojia hiyo haijamfikia mkulima.
Alisema wananchi wote wakielewa vizuri jambo hili litasaidia kuondoa mashaka juu ya usalama wa teknolojia ambao umekuwa ukitolewa na watu mbalimbali na mashaka hayo yakiondoka ndipo sasa kila mtu anaweza kuwa huru kuchagua kuitumia teknolojia hiyo au la kwa manufaa yake na manufaa ya taifa kwa ujumla.
Profesa, Kamata aliongeza kuwa mashaka ni lazima kwa jambo lolote au teknolojia yoyote mpya inapoingia sokoni na huu ndio wakati muafaka wa watafiti kusikia mashaka na watu na kisha kuyatafutia majibu ya kisayansi kwani hakuna mtu anayeweza kufurahia jambo bila kuwa na wasiswasi hususani kwa teknolojia mpya yoyote.
Awali akiwasilisha mada yake ambayo ilitakiwa kujibiwa na Dkt. Nyange dhidi ya GMO mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaamu, Richard Mbunda alisema bado kuna taarifa ambazo zinapishana katika kiwango ambacho mbegu za GMO zinazostahimili ukame ambazo zinefanyiwa majaribio kwenye kituo cha utafiti wa kilimo makutupora katika uwezo wake wa kupunguza hasara kwa mkulima.
Mbunda amesema mashaka makubwa wanayoyaona baadhi ya watu ni kuhusu usalama wa vyakula vinavyotokana na mbegu za GMO kama chakula kwa maana ya afya na mazingira mambo ambayo ni lazima watafiti wayaangalie na kujiridhisha kabla ya kuzipeleka mbegu hizo kwenye mamlaka za serikali zinazopitisha mbegu zote nchini.
Mtoa mada huyo alieleza wasiswasi wake na kutaka kujua juu ya namna mkulima mdogo atakavyoweza kunufaika na teknolojia hiyo ili isijemfanya mkulima kuwa mtegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi na kutaka kujua namna wakulima watakavyoweza kupata mbegu hizo kwa urahisi na bei nafuu pale ambapo zitapitishwa na kuwa mbegu ili kutumika hapa nchini.
VIONGOZI WA CHADEMA WAACHIWA KWA DHAMANA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wachama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa 6:50 mchana
Viongozi hao walifika kituoni hapo leo Jumanne Februari 27, 2018 na kuachiwa saa 1:02 usiku, kuitikia wito wa polisi.
Walikwenda kituoni hapo baada ya Mbowe kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni.
Mmoja wa mawakili wa viongozi hao, Frederick Kihwelo ameileza MCL Digital leo kuwa wote wameachiwa kwa dhamana kwa kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 5, 2018 saa 1 asubuhi.
Amesema viongozi hao walianza kuhojiwa saa 8:30 mchana, baada ya kufanya mazungumzo ya tuhuma zinazowakabili.
Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.
Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.
Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.
Viongozi wengine waliohojiwa sambamba na Mbowe ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.
Mdee, Matiko, Heche na Mnyika walisharipoti awali na walitakiwa kurejea kituoni leo. Viongozi wengine waliwakilishwa na wanasheria.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji hakwenda polisi kwa kuwa yupo nje ya nchi
FATUMA KARUME APINGA VIKALI CHAGUZI KUSIMAMIWA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI
Kufuatia zoezi la usimamizi wa kura za majimbo kusimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya Mwanasheria Fatma Karume ameibuka na kupinga vikali utaratibu huo.
Katika sakata hilo la kupinga wakurugenzi hao ambao ni wateule wa Rais Magufuli kushiriki kwenye usimamizi wa Chaguzi hizo, fatma karume atasaidiwa na Mtoto wa aliyekuwa Mbunge Tarime Chacha Wangwe, Bob Wangwe pamoja na mashirika yanayotetea haki za binadamu.
Akiongea na waandishi wa habari mapema jana Fatma Karume amesema kuwa Tanzania sasa baadhi ya viongozi waliwahi kusikika wakijinadi kushinda uchaguzi hata kwa magoli ya mkono na kudai kuwa haki ya kura sasa inaonekana kama haina thamani, hivyo wao wanataka kuipigania haki hiyo kupitia sheria ili ipatikane.
Aidha Fatma Karume amesema watu ambao waliweka mfumo huo wa Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa na lengo lao na walifanya hivyo kwa kuwa walikuwa wanajua nini wanataka kufanya.
"Mtu akipiga kura haina thamani yoyote na matakwa yake hayasikilizwi kwa sababu kuna kitu kinaitwa goli la mkono, sasa kama kuna goli la mkono linatoka kwenye mfumo, kama kwenye mfumo kuna refa anaona, refa wa haki hawezi kukubali goli la mkono lakini tukajiuliza ni nini kinafanya refa afunge macho au asione watu ambao wanasema wao watashinda kwa goli la mkono. Kila mtu ana haki ya kupiga kura na kura yake ihesabike sasa kama kuna watu wanapiga magoli ya mkono haki yako hii inachukuliwa yaani imetekwa"
"Chini ya Katiba yetu refalii wa masuala haya ni Tume ya Uchaguzi, Katiba inasema huyo refalii lazima awe mtu ambaye hayumo kwenye chama chochote cha kisiasa siyo CHADEMA, CCM wala CUF bali anatakiwa awe mtu ambaye si mwanachama wa chama chochote, kwa hiyo msimamizi wa uchaguzi ni marufuku kuwa chini ya chama chochote kwa mujibu wa Katiba yetu yaani kuna matatizo makubwa ya sheria hapa lakini mwisho unakuta unakuta kwamba wasimamizi wa kura wanavaa magwanda ya chama siku moja siku ya pili wanavaa sare za Tume ya Uchaguzi na wananchi wanalalamika kwa sababu ya mfumo na mfumo umewekwa kisheria na watu walioweka huo mfumo wanajua wamefanya nini" alisema Fatma Karume
Kufuatia mapungufu hayo ya Sheria Fatma Karume amesema kuwa alichokigundua yeye magoli ya mkono yanatokea kwa sababu ya mfumo na kwa mfumo huo hizo kura zitapigwa kila siku hivyo ameshauri waende mahakamani kuhoji mahakama kama mfumo huo unakubalika chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataka kila kura ihesabike, na katiba inayotaka Demokrasia
Tuesday, February 27, 2018
ANGALIA HAPA KUJUA KILICHOTOKEA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UONGOZI
Wanawake
kote nchini wametakiwa kuacha tofauti zao, wakae pamoja na kuangalia changamoto
zinazowakabili na watafute namna ya kuzitatua ili waweze kusonga mbele.
Hayo yamesemwa
mapema leo jijini Dar es salaam na Mh. Merry Nagu alipokuwa akifugua kongamano
la siku moja la wanawake na uongozi lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia TGNP.
Kongamano
hilo lililofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam liliudhuliwa na
watu wengi mashuhuri na wenye mchango mkubwa kwa taifa kama Mama Anna Makinda,
Marry Rusimbi, Ester Bulaya Prof. Ruth Meena nk.
Katika
kongamano hilo Marry Nagu alipenda kuwashauri kwa wale wanawake waliopata
nafasi nzuri waweze kuzitumia nafasi hizo katika kuwanufaisha wanawake wenzao
kama alivyofanya yeye.
“Wanawake wenye
nafasi nzuri katika uongozi mnatakiwa kuzitumia nafasi hizo kuwakomboa wanawake
wenzenu kama nilivyofanya mimi nilipokuwa Waziri wa Utumishi kwa kuweza kubadilisha
sharia ya utumishi kutoka sharia ya serikali mchakato kwenda serikali matokeo”
alisema Marry Nagu
“Katika
ushiriki wa wanawake kwenye uongozi bado kuna changamoto katika kuchaguliwa au
kupigiwa kura lakini wanawake tunatakiwa kuonyesha kwamba tunaweza na tuweze
kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe, kwani hii itawapa msukumo hata wanaume kuweza
kutupigia kura kwa kuona umoja wetu” alisema Marry Nagu
Aidha Marry
Nagu alipenda kuwashauri wanawake kuwa haitoshi kwa kusema wao ni wachakalikaji
au wabangaizaji kwani mwisho wa siku wanakuwa hawana chochote wanachokipata na
hivyo wanatakiwa kuwa wajasiliamari ili kujiongezea kipato katika maisha yao ya
kila siku.
Na mwisho
kabisa alipenda kumpongeza Rais Magufuri kwa kuona mchango na umuhimu wa
wanawake katika serikali yake hata kumchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa
makamu wake, hii inaonyesha kwa kiasi gani rais anasogeza mbele harakati za
wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo katika Kongamano la Wanawake na Uongozi lililoandaliwa na Mtandao huo Mlimani City jijini Dar es salaam. |
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema kuwa lengo la Kongamano
hilo ni kujumuika, kushauriana/ kuelimishana kuhusu changamoto mbalimbali
zinazowakabili wanawake kote nchini.
Mkurugenzi huyo
aliendelea kusema kuwa bado wanawake hawapewi nafasi ipasavyo kwani takwimu
zinaonyesha kuwa hadi kufika oktoba 11 2017 wanawake waliyoweza kushika
madaraka kama wakuu wa nchi ni 11 kati ya 178 na kwa afrika ni mwanamke mmoja
tu ndio kiongozi wa juu yaani Rais.
Lakini pia Rwanda
imekuwa ya kwanza kwa afrika mashariki na kidunia kwa asilimia 61.3 na Tanzania
imekuwa ya pili kwa Afrika Mashariki lakini ya 25 kidunia kwa kuwa na asilimia
36.9 hivyo hali bado siyo nzuri katika usawa wa kijinsia.
Aidha Mkurugenzi
huyo aliendelea kusisitiza swala la wanawake kuwezeshwa kiuchumi hii ikiwa ni
pamoja na kazi za huduma ambazo zimekuwa ni kama majukumumu ya kawaida kwao
bila kupata kipato chochote, wakati muda huo wangeutumia kutafuta kipato
wengeweza kujenga uchumi wa nchi.
Na mwisho Lilian alipenda kushauri kuwa wanawake wapewe nafasi katika uongozi na maamuzi ili waweze kuonyesha uwezo wao katika Nyanja hizo kwani ushiriki wao umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na wanaume kama wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa.
Na mwisho Lilian alipenda kushauri kuwa wanawake wapewe nafasi katika uongozi na maamuzi ili waweze kuonyesha uwezo wao katika Nyanja hizo kwani ushiriki wao umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na wanaume kama wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa.
Wageni mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake na uongozi lililoandaliwa na TGNP Mtandao mapema leo jijini Dar es salaam |
Subscribe to:
Posts (Atom)