SERIKALI imetakiwa kuzitambua kazi za kutoa huduma zinazotekelezwa na wanawake na kuziingiza katika Mipango ya Taifa kwani zinaweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa
mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TGNP)
Bi. Lilian Liundi alipokuwa akitoa Mhuktasari wa Kongamano la Wanawake na Uongozi.
Kongamano hilo
linatarajiwa kufanyika siku ya jumanne ya tarehe 27 Mlimani City jijini Dar
es salaam, likihudhuliwa wanawake mbalimbali walio katika nafasi za uongozi na
waliostafu.
Mkurugenzi huyo
alisema kuwa kuna haja ya serikali kuzitambua shughuli mbalimbali zinazotolewa
na wanawake kama huduma kwa lengo la kujipatia kipato kwani uchunguzi umebaini
kuwa wanawake hutumia muda wa masaa 10 mpaka 15 kwa siku kwa shughuli hizo
hivyo wanakosa muda wa kufanya shughuli za kujipatia kipato.
Aidha Mkurugenzi
huyo aliendelea kusema kuwa lengo kuu la Kongamano hilo ni wanawake kwa pamoja kuweza
kujadili namna gani wataweza kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwani bado
hawajaweza kufikia lengo ambalo ni 50 kwa 50.
Lakini pia
kuweza kusherekea, kupongezana na kuajadili changamoto mbalimbali anazokutana
nazo mwanamke katika Nyanja ya elimu, afya na umiliki wa ardhi swala ambalo
bado ni changamoto kubwa kwa wanawake wengi hivi sasa.
Bi. Lilian aliendelea
kusema kuwa kutakuwa na kuenzi na kukumbuka mchango uliotolewa na wanawake
ambao walikuwa katika ngazi za uongozi maamuzi kuanzia ngazi ya jamii mpaka taifa.
Mgeni Rasmi
katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri msataafu Mama Marry Nagu, lakini
pia kutakuwa na wadau zaidi ya 250 wanawake kwa wanaume viongozi wa sasa na
wastaafu katika kuhakikisha kongamano hilo linaleta tija kwa jamii yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano na waandishi kuhusu kongamano la Wanawake Uongozi. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi wa katikati akiwa na jopo la wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika kuandaa Kongamano la Wanawake na Uongozi. |
Waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao. |
ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI KUHUSU KONGAMANO HILO....
No comments:
Post a Comment