Wateja 156 wa Tigo wajinyakulia smartphone za TECNO R6 4G
Zaidi ya simu 900 na bonasi za internet bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Februari 26, 2018 – ‘Kwa sasa mama yangu
anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi kuwasiliana kikamilifu kwa njia ya
mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia picha za wajukuu wake. Ndio maana nitampa zawadi ya simu hii mpya niliyoshinda
kutoka Tigo leo ili iturahisishie mawasiliano yetu na kumfanya awe sehemu ya
ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni maneno ya Margareth Martin Hiza,
mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka moja wa
washindi wa simu mpya za kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 4G katika
promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo Tanzania.
Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo
bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya
kushinda mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka
Nyaka Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi
vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwaya *147*00#.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa wiki hii, Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna zaidi ya simu 900
aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G ambazo zinashindaniwa na wateja watakaonunua
vifurushi vya intaneti vya kuanzia TSH 1,000 kupiita menu *147*00#.
‘Washindi wetu wote 156 tuliowapata kufikia sasa wanatoka
sehemu mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini
washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi
ya 900 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Woinde alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza
idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments:
Post a Comment