MBUNGE wa Jimbo la Kibamba na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema jeshi la polisi lisipowapatia dhamana leo wananchi 40 waliokamatwa katika maandamano ya Februari 16 mwaka huu wakati wakielekea ofisini kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kinondoni kuanzia kesho, wataenda mahakamani kwa ajili ya kupatiwa sheria inayoruhusu jeshi la polisi kuwashikilia kwa muda wote huo.
Amesema kuwa kitendo cha jeshi la polisi kuwashikilia kwa muda wote huo ni ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu, hivyo chama chao kipo tayari kufungua kesi dhidi ya polisi.
Mnyika alifafanua kwamba wamefanya uchunguzi na wamebaini miongoni mwa wananchi hao waliokamtwa si wafuasi wa Chadema bali raia waliokuwa wakipita njiani na kukumbwa na balaa hilo ambapo wengine ni watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka 18.
No comments:
Post a Comment