KALI YA MWAKA! Hili linaweza kuwa ni jambo la kushangaza kutokana na ugumu wa asilimia kubwa ya wanawake kushindwa kukubaliana na uhalisia juu ya sheria ya Dini ya Kiislam inayouhusu mume kuoa mke zaidi ya mmoja.
Jambo hilo limekuwa jepesi kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Bi. Zainab Abdallah ambaye ameushangaza umma baada ya kumruhusu, kumuandaa na kumpongeza mumewe kwa kuongeza mke wa pili.
Bi. Zainab ambaye ni mkuu wa wilaya mdogo kuliko wote nchini Tanzania ni mke halali wa Abdul Mohamed ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, walifunga ndoa takribani miezi 7 iliyopita.
DC huyo amezitoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa wa Instagram na kuweka picha ya Bi. Harusi na Mumewe baada ya kufunga ndoa na mke mwingine.
“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu @vanmohamed kwa kuongeza Mke wa Pili. Kwa kuwa dini yetu ya kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi.
Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu @only_chibeb wa kusaidiana nae majukumu mazito ya ulezi wa mume.
Alhamdulillah, M/Mungu ametupa rizki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.
Alhamdulillah, M/Mungu ametupa rizki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.
Karibu sana kwenye familia @only_chibeb nimekupokea kwa mikono miwili na inshaaAllah M/Mungu atupe maskilizano na tuishi na mume wetu kwa wema till Jannah InshaaAllah.
Baaraka llahu lakumaa, wabaraka alaykumaa, wajamaa baynakumaa fil khaeyr
No comments:
Post a Comment