Monday, February 19, 2018

CHADEMA YATOA RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA KIONGOZI WAO ALIYEUWAWA KWA KUTEKWA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kinatarajia kuongoza shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Hananasif Jimbo la Kinondoni, Daniely John siku ya kesho (Jumanne).
Picha inayohusiana
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene jioni ya leo (Jumatatu) na kudai mwili wa marehemu Daniel unatarajiwa kufika nyumbani kwake Hananasif ukiwa unatokea hospitali ya Taifa Muhimbili majira ya saa 4 asubuhi na kisha kupelekwa katika Kanisa la Katoliki kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu itakayoanza saa 5 asubuhi kanisani hapo.

Baada ya ibada hiyo, waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho kwa Daniel kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa siku ya Jumatano, katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.

Kwa taarifa kamili soma hapo chini.

No comments: