Aidha ugeni huo wa Meya wa Jiji la Blantyre ulihusisha madiwani watatu, Balozi mdogo wa Maalawi Sai Kaphale ambapo wote walipata fursa ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART).
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufanya mazungumzo hayo, Meya Mwita amesema lengo la ugeni huo ni kuendeleza urafiki ambao utawezesha kubadilishana ujuzi kwenye uendeshaji wa majiji hususani kwenye miundombinu ya Elimu, barabara ,Utalii na huduma nyingine za kijamii.
Amesema kuwa wakiwa jijini hapa watajifunza namna ya kuendesha miundombinu hiyo hususani ya Barabara na Elimu ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam limepata mafanikio makubwa kwenye utoaji wa huduma hizo.
Ameongeza kuwa mbali na miundombinu hiyo, lakini watapa fursa ya kujifunza namna ya ukusanyaji kodi na kuongeza mapato kwenye jiji ambapo kesho watashiriki kwenye baraza la Bajeti litakalokaa siku mbili.
Kwaupande wake Meya wa Jiji la Blantyre Wild Ndipo amefurahia mapokezi waliyopata kutoka kwa Meya Mwita na kuahidi kushirikiana na jiji la Dar es Salaam katika masuala mbalimbali ya maendeleo
ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI..
No comments:
Post a Comment