Wateja
wa Tigo kupata faida mara tatu kupitia promosheni za kusisimua
Mtwara,
Oktoba 13, 2018 – Huku
msimu wa mavuno ya korosho ukiwa umewadia katika mikoa ya nyanda za juu kusini,
wakaazi wa Mtwara na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama lote kutoka kwa
mastaa wa muziki wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta 2018 –
Vibe Kama Lote.
Waandaaji Clouds Media Group, kupitia
Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner Habash amewaalika wakaazi wa
Mtwara waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna korosho kwa kusikiliza
100% vibe za nyumbani.
‘Kwa wafanya biashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni
fursa ya kujiongezea kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na
chakula na huduma nyingenezo zinazohitajika na maelefu ya mashabiki
watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius
Byanakwa alisema.
Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 –
Supa Nyota, wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara watapata nafasi ya kuonesha
vipaji vyao, na wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya kutumbuiza katika
tamasha kuu la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima siku
ya Jumapili tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.
‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza
kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua
kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa
mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa
4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza
kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama
zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki
katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa
kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.
Watakaoshusha vibe kama lote mjini
Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii
(Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki
mjini Iringa. Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge,
Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.
TIketi
za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo
Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#,
kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass).
Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda
namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe
Kama Lote tayari limezuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa, na
linatarajiwa kutembelea mikoa ya Singida,
Songea, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku
fainali ikiwa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment