Tuesday, February 13, 2018

LHRC YAJA NA HII KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SOMA HAPA KUJUA..

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa utendaji wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikidai  umegubikwa na ukiukwaji utawala wa sheria kwenye utekelezaji wa majukumu yake.
Tokeo la picha la LHRC
Hatua hii ya LHRC inakuja siku chache baada ya mkuu huyo wa mkoa kusimamisha utendaji wa mabaraza ya ardhi ya kata kinyume na sheria pamoja na kudaiwa kuingilia muhimili wa mahakama katika mkutano baina yake na wakazi wa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Felista Mauya amesema kupitia utendaji kazi wa serikali kumekuwepo na juhudi mbali mbali za kuboresha ustawi wa maisha ya wananchi ikiwemo kuwakutanisha wananchi, kuwasikiliza na kuweka mikakati bora ya kutatua kero zao.

“Hata hivyo ombwe la viongozi wa serikali kutofuata taratibu na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao limeendelea kuathiri uhalali wa juhudi hizo,” amesema Mauya.

Ameongeza “Kupitia mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wananchi wa Dar es Salaam uliofanyika Februali 10, 2018, LHRC kimebaini mapungufu kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa si tu na Paul Makonda pekee bali pia na baadhi ya viongozi wengine wa serikali baadhi ya mapungufu ya kisheria yanayotokana na mkutano huo ni pamoja na kusimamisha utendaji wa mabaraza ya ardhi ya  kata kinyume na sheria na kuingilia muhimili wa mahakama."

Mauya amewakumbusha viongozi wa serikali na wanasiasa kuwa hawana mamlaka ya kisheria kuingilia utendaji kazi wa mahakama wala kuelekeza utendaji wa mahakama badala yake wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu za kimahakama katika upatikanaji wa haki.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Felista Mauya, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam leo.

Kutokana na mambo hayo yote kituo cha sheria na haki za binadamu kimetoa mapendekezo mengi na baadhi ya mapendekezo hayo ni.

Serikali kufuata taratibu za kiseheria katika kutatua kero na changamoto mbali mbali, watendaji wa serikali hasa katika nafasi za kisiasa wanapaswa kuachakutumia mbinu za kisiasa, badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo kisheria ili kutatua changamoto na kero za wananchi kwa maendeleo endelevu.

Viongozi wa kisiasa kuacha kutumia mamlaka yao majukwaani kuwajibisha watumishi wa umma badala yake kufuata taratibu kama zilivyoainishwa katika sheria ya utumishi wa umma ya 2002.

Watendaji wa serikali kuheshimu muhimili wa mahakama, viongozi wa serikali wameapa kulinda katiba kupitia Ibara 107 inaipa mahakama mamlaka  ya juu katika kutenda haki.

No comments: