Mwanahabari Patrick Mwillongo enzi za uhai wake
Ndugu zake marehemu Patrick Mwillongo wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao iliyofanyika nyumbani kwao Kiburugwa Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
Ibada ikiendelea.
Waombolezaji wakifuatilia ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Yusuph Peter wa Kanisa na Tanzania Assemblies of God Kingugi jijini Dar es Salaam, akiongoza ibada hiyo.
Mjane wa marehemu Theresia Conrad akiwa mwenye majonzi kwa kuondokewa na sukari yake mmewe.
Huzuni katika ibada hiyo.
Dada wa marehemu akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa mdogo wake.
Mwanahabri Careen akitoa heshima za mwisho. Kushoto ni mwanahabari Kulwa Mwaibale.
Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa. Wa pili kutoka kushoto ni Mwanahabari Dotto Mwaibale na wa tatu ni Kulwa Mwaibale.
Msafara kuelekea makaburini Chang'ombe ukianza kutokea nyumbani kwao marehemu.
Jeneza likishushwa kaburini.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa baba yao.
Mwanahabari Kulwa Mwaibale akiweka shada la maua katika kaburi la Mwillongo.
Baadhi ya waaandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mjane wa marehemu.
Na Dotto Mwaibale
MAJONZI, vilio na simanzi vilitawala wakati wa ibada ya kumuaga Mwanahabari Patrick Mwillongo aliyefariki dunia Machi 12, mwaka huu katika Hospitali Ndogo ya Muhimbili ya Mloganzila iliyopo Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu na mazishi yake kufanyika katika makaburi ya Chang'ombe Maduka Mawili.
Akizungumza wakati akitoa mahubiri katika ibada hiyo iliyofanyika jana, Mchungaji Yusuph Peter wa Kanisa na Tanzania Assemblies of God Kingugi aliwakumbusha watu wote waliokuwepo kwenye ibada kujiandaa kwa maana hawajui ni lini watafikwa na mauti.
"Mwenzetu Patrick Mwillongo atunaye tena amekufa sasa sisi tulio hai kwa dini zetu tunapaswa kujitafakari kwa kuacha dhambi na kutubu" alisema Peter.
Katika ibada hiyo na mazishi ya Mwillongo yalihudhiriwa na baadhi ya waandishi wa habari wasiozidi 10, Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Wilaya ya Bagamoyo, Hemed Kipozi na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mwillongo.
Marehemu Patrick Mwillongo aliyezaliwa mwaka 1975 enzi za uhai wake alikuwa akiandikia magazeti ya Mtanzania na Jambo Leo na ameacha wajane na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Katika tukio la kusikitisha usiku wa kuamkia leo vibaka walivamia katika msiba huo nyumbani kwao marehemu Kiburugwa na kufanikiwa kuiba mikoba ya wafiwa iliyokuwa na simu na vitu vingine.
Katika tukio la kusikitisha usiku wa kuamkia leo vibaka walivamia katika msiba huo nyumbani kwao marehemu Kiburugwa na kufanikiwa kuiba mikoba ya wafiwa iliyokuwa na simu na vitu vingine.
No comments:
Post a Comment