Wednesday, February 7, 2018

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM KIBAHA MJINI EDWINI SHUNDA APOKEA WANACHAMA KUMI WA UPINZANI KATA YA MBWAWA.






   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda akifyeka kusafisha mazingira ya zahanati ya Mbwawa.





 Ukaguzi ukiendelea



 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mbwawa,Hoja Said akizungumza katika mkutano huo.

 Ukaguzi wa vyoo vya Zahanati ya Miswe ukiendelea.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda akimkabidhi kadi ya chama hicho,Mlokote Iddy (kulia) katika maadhimisho ya miaka 41 ya CCM ya Kata ya Mbwawa jana.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kata ya Mbwawa,Illuminata Makwaya.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda akiwaongoza wananchama wapya 10 kula kiapo cha kuitumikia chama hicho.


Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mbwawa Illuminata Makwaya akizungumza katika mkutano huo.
 NA ELISA SHUNDA,KIBAHA 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini kupitia kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa wilaya hiyo,Edwin Shunda, kimepokea wanachama 10 wa vyama vya upinzani 7 kutoka Chama cha ACT Wazalendo na 3 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM tangu kuanzishwa kwake katika kata ya Mbwawa jana. 
Uongozi wa chama hicho na wanachama waliadhimisha sherehe hizo kwa kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka na kufagia katika maeneo yanayoizunguka zahanati ya Miswe na Mbwawa pamoja na kuangalia mradi wa ujenzi wa shule ya awali katika kijiji cha Mkoleni.
Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda aliwaambia wanachama hao wasifanye kazi siku hiyo tu kwa ajili kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa chama hicho bali ikiwabidi wapange ratiba kila baada ya muda Fulani wafanye usafi katika taasisi mbalimbali za serikali na jamii ili kuwa mfano mzuri wa kuigwa pamoja na kumsaidia Rais Dk.John Magufuli kwa kupitia katika taasisi hizo ili kuangalia changamoto zilizopo na kuzitatua pale inapobidi au kupeleka taarifa halmashauri ili washughulikie changamoto.
“Nimefurahishwa na usafi wa mazingira tuliofanya wote kwa siku ya leo ila nawaomba isiwe leo tu tupange muda wa kufanya usafi mara kwa mara katika taasisi hizi pamoja na kuisaidia serikali kupitia kwa Rais Magufuli kwa kutatua au kuangalia changamoto zilizopo katika kata yetu na kuziwasilisha kwa mkurugenzi wa halmashauri ili zitatuliwe” Alisema Shunda
Aidha mwenyekiti huyo aliwaambia wao ni mashahidi wametembelea zahanati hizo na kujionea changamoto zilizokuwepo ikiwemo baadhi ya vipimo vinapimwa na zahanati binafsi wakati kama taarifa ikipelekwa halmashauri wanaweza kushughulikia kero hiyo na kuwakumbusha kwa kuwaambia Rais Magufuli amerudisha imani ya wanachama wengi wa vyama vya upinzani kwa kutekeleza kero za jamii pamoja na kupigana kuondoa ufisadi ndo maana hata wanachama kumi wameweza kujiunga na chama hicho siku hiyo kutokana na kuwa na imani ya chama hicho kulingana na matendo uchapaji kazi wa serikali ya awamu ya tano hivyo ni jukumu lao viongozi kufanya kazi kwa vitendo.
“Hawa  wenzetu wameamua leo (jana) kuludi katika chama tawala kulingana na utendaji kazi na imani yao kwa rais magufuli na kuona udhaifu wa upinzani kwa mfano hapa Kata ya Mbwawa Diwani Rajab Kombe wa kutoka ACT Wazalendo tangu achaguliwe wananchi wanalalamika kutoka na utendaji kazi wake kutokuwa na kasi na tija kama ya CCM hivyo naamini ikifika mwaka 2020 hamtorudia tena makosa” Alisema Shunda
Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mbwawa Illuminata Makwaya alisema kuwa wanambwawa wanajuta kwa nini walimchagua diwani wa upinzani kutokana na kuzorota kwa maendeleo katika kata hiyo na pia watahakikisha wanatatua au kufikisha changamoto zitakazojitokeza katika kata hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wapya waliojiunga na CCM kutokea upinzani,Mlokote Iddy alisema kuwa wameamua kuludi katika chama hicho kutokana na sasa hivi utendaji wa serikali ya awamu ya tano kuwaridhisha tofauti na hapo awali watendaji walikuwa kama miungu watu wanafanya kazi vile wapendavyo ila kwa sasa heshima ya kazi imeimarishwa na Rais Dk.John Magufuli.

No comments: