Wednesday, February 7, 2018

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA KIBAHA MJINI AMEWASHAURI VIJANA KUPENDA MICHEZO KWA AFYA YA MWILI NA KUCHANGAMSHA AKILI.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda akipimana ubavu na Onesmo Cornely (kulia) katika mchezo wa Drafti alipotembelea katika Kata ya Mbwawa,jana kwa ajili ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wanaoshuhudia Katikati ni Mwenyekiti wa chama hicho kata hiyo,Illuminata Makwaya na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa kata hiyo,Ally Bwida. Picha na Elisa Shunda 


NA ELISA SHUNDA KIBAHA
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda amewashauri vijana kupenda kufanya mazoezi ya mwili kwa kushiriki katika michezo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya ya mwili na kuchangamsha ubongo kufikiri na kufanya  kazi kwa haraka lakini pia kujiepusha na maradhi mbalimbali yanayosababishwa na kuwepo kwa mafuta uzembe katika mwili.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti huyo wakati alipowatembelea vijana eneo la sokoni katika kata ya Mbwawa wilayani Kibaha jana kwenye maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwakuta wakicheza mchezo wa drafti  na kushiriki nao kwa kucheza ambapo aliwashauri kutengeneza club za mchezo huo na kutengeneza ligi itakayowapa motisha hata vijana wengine na wananchi wa kata hiyo kuandaa ligi mbalimbali za michezo ikiwamo na mchezo unaopendwa na watu wengi wa mpira wa miguu.

“Ili kijana ujiepushe na mambo yasiyomema na fikra mbaya katika ubongo wako kuna baadhi ya sehemu ni lazima ujikite nako ikiwemo sekta ya michezo ambayo itakufanya uimarishe afya yako lakini pia itakufanya ufikirie kwa haraka na kufanya maamuzi sahihi nawaona hapa vijana mnacheza drafti hapa ni mchezo mzuri sana unatumia akili nyingi kufikiria hivyo unaufanya ubongo wako uchangamke tofauti na kukaa vijiweni mtaongopeana mambo mbalimbali ikiwemo na kushawishiana kutenda mambo yasiyopendeza katika jamii inayowazunguka” Alisema Shunda

Aidha Mwenyekiti Shunda aliwaambia vijana hao kuanzisha ligi ya Drafti ambayo itakuwa inashirikisha vijana wa mitaa yote ya kata hiyo lakini pia itaamsha morali na kwa wapenzi wa michezo mingine kuanzisha ligi zao ukiwemo mchezo unaopendwa na watu wengi wa mpira wa miguu.

Aliongeza kwa kuwaambia hata yeye katika kata yao ya Kongowe akishirikiana na wadau wa michezo walianzisha ligi ya mpira wa miguu ambayo ilipendwa na kutazamwa na wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali iliyokuwa ikiitwa Shunda Cup lakini pia kutokana na ligi hiyo kuvutia hata waandishi wa habari za michezo akiwemo marehemu Justine Limonga wa Radio Uhuru na wengineo walikuwa wakija kushuhudia ligi hiyo pamoja na kuitangaza na baadhi ya vijana walioshiriki ligi hiyo walipata nafasi katika timu zilizokuwa zikishiriki ligi daraja la kwanza na ligi kuu.

No comments: