Wednesday, February 21, 2018

RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Rais John Magufuli leo amewasili nchini Uganda, kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaofanyika  mjini Kampala.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe, Rais Magufuli amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa na kisha kuelekea Ikulu ya Entebbe.

Baada ya kuwasili Ikulu amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda  Yoweri  Museveni.

Pia kesho atahudhuria mkutano maalum katika ngazi ya wakuu wa nchi unaohusu masuala ya miundombinu na afya na keshokutwa atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments: