Friday, February 16, 2018

WATANZANIA WAWILI MKE NA MUME WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA, MTOTO WAO ARUDISHWA LEO NCHINI

WATANZANIA wawili mume na mke waliotambulika kwa majina ya Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa wamekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, China,  wakiwa na mtoto wao mdogo wa miaka miwili ambaye amerudishwa nchini Tanzania, jana Feb. 15, 2017.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Sheria za Madawa ya kulevya, Edwin Kakolaki, amesema raia hao wa Tanzania Januari 19, 2018 wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Baiyun Guangzhou, walikamatwa wakiwa wamemeza (tumboni) dawa za kulevya, ambapo  baadaye Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja kubwa na mkewe  pipi 82.


Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha nchini ambapo aliwasili jana na Serikali ikafanya utaratibu wa kuwatafuta ndugu zake kwa ajili ya malezi na matunzo.

Akizungumzia kuhusu idadi ya Watanzania  walioko  magerezani nchini China kwa tuhuma za madawa ya kulevya, amesema wapo zaidi ya Watanzania 250  na wanafuatilia zaidi ili kupata idadi yao kamili.

No comments: