Friday, February 16, 2018

AHADI ZA DKT. SLAA KWA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUAPISHWA

Tokeo la picha la KUAPISHWA KWA DKT SLAA
IKIWA ni dakika chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuwaapisha Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Slaa amefunguka kuwa hatomuangusha Rais na badala yake atajituma kwa nguvu zake zote kulitumikia taifa kwa manufaa ya nchi.

“Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu, pia nikushukuru Rais Magufuli kwa kunichagua kulitumikia Taifa, wewe unafahamu vigezo ulivyotumia kuniteua.
“Ninakuahidi nitafanya kazi yangu kwa moyo wangu wote, akili yangu yote na kwa nguvu zangu zote ili kujenga uchumi wa kati wa nchi yetu, Mwenyezi Mungu akinisaidia pia nikishirikiana na timu ya wote. Mimi katika siasa zangu sijawahi kutoa ahadi, lakini leo naweza kusema tu kwamba sitokuangusha,” alisema Dkt. Slaa

No comments: