Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana walipotembelea Bohari ya Dawa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula, akitoa maelezo kwa wanahabari jinsi vifaa tiba na dawa zinavyohifadhiwa katika bohari hiyo.
Muonekano wa maboksi ya dawa jinsi yalivyopangwa ndani ya bohari iliyopo Makao Makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam.
Dawa na vifaa tiba zikipelekwa kuhifadhiwa ndani ya bohari.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akiwaonesha waandishi wa habari vifaa mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula na Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia, akiwaonesha wabahabari vifaa vilivyopo kwenye mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Hilda Mhagama kutoka gazeti la Daily News.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Saum Juma kutoka Kituo cha Televisheni cha TV One.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imezidi kuboresha huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hata kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa na kupata ithibati ya ISO 9001:2015.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED ilifanya ukaguzi Makao makuu ya MSD pamoja na Kanda zake nane mwezi Agosti 2017 na MSD ilionekana kufuata miongozo ya juu ya kimataifa na matakwa ya mamlaka za udhibiti ubora nchini.
Katika mkutano huo, Bwanakunu pia alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu(135) MSD imeimarika na kufikia asilimia 90,huku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini hali ya upatikanaji wa dawa ni kati ya asilimia 85 na 98.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD pia aliwaonyesha waandishi wa habari Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000.
Amesihi taasisi, asasi, jumuiya na wananchi kununua mifuko hiyo ya vifaa vya kujifungulia na kutoa msaada kwenye vituo vya afya na hospitali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya nchini .
Katika mkutano huo Bwanakunu aliwazawadia waandishi wa habari wawili ambao ni wajawazito mfuko huo wa vifaa vya kujifungulia kwa ajili ya kujiandaa kwenda kujifungua.
1 comment:
Hello mate great blogg post
Post a Comment