Ikiwa ni wiki Kadhaa kupita Tangu kumalizika kwa
uchaguzi Mdogo wa Ubunge kwa majimbo mawili ya Kinondoni na Siha uchaguzi ambao
Chama cha mapinduzi CCM waliibuka kidedea hatimaye ripoti ya Kituo cha sheria
na haki za Binadamu kuhusu uchaguzi huo imeeleza wazi kuwa pamoja na kuwa
uchaguzi huru lakinu haukuwa wa Haki..
Mapema Leo makao makuu ya ya kituo hicho Dar es
salaam Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Anna Henga amesema kuwa uchaguzi huo uligubikwa
na kasoro nyingi ikiwemo vyama vya upinzani kuminywa haki zao za msingi huku
chama Tawala kikizipata.
Henga amesema kuwa sakata la Kuzuiwa kwa Mawakala wa
vyama vya upinzani kuingia katika vituo vya kupigia kura na kuchelewa kuingia
ni moja kati ya dosari kubwa zilizouharibu uchaguzi huo na kuonekana ni
uchaguzi wa Upande mmoja ambapo mawakala wa chama Tawala hawakupata usumbufu
wowote.
Aidha amesema kuwa swala lilingine lililotia dosari
katika uchaguzi huo ni Matumizi makubwa ya nguvu yaliyopelekea kujeruhiwa kwa
baadhi ya wananchi na Kifo cha mwanafunzi Akwilina ambapo wamesema kuwa
hakukuwa na ulazima wa kutumia nguvu katika uchaguzi huo.
Akifafanua report hiyo Henga ameweka wazi kuwa Kituo
cha sheria na Haki za Binadamu LHRC sio mshirika wa vyama vya upinzani bali
wanasimamia sheria na pale kwenye ukweli lazima usemwa kwa kuwa ni haki za watu
zimeminywa.
“Wanasema sisi ni wapinzani lakini sio kweli hii ni
kwa kuwa tunaongea ukweli,sisi ni watu huru tunaopogania haki za binadamu na
hatutaogopa kwa kuwa tupo ndani ya sheria za nchi na hatuvunji sheria” Ameeleza
Kaimu Mkurugenzi huyo Anna Henga.
Maswala mengine yaliyotajwa na kituo hicho kama
dosari katika uchaguzi huo ni pamoja na Mwitikio mdogo wa wapiga kura,Vituo
kutofunguliwa kwa wakati,Uwepo wa polisi wengi vituoni,Matumizi ya watoto
katika kampeni akitolea mfano video iliyosambaa ikionyesha motto akicheza
jukwaani katika kampeni ya Chama cha mapinduzi kinyume na sheria za
uchaguzi,Pamoja na matumizi ya Rasilimali za Umma katika kampeni huku akiwataja
baadhi ya mawaziri kutumia magari ya serikali katika kampeni za uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment