Friday, March 2, 2018

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA 2018 NI MOTO, WAIMBAJI BEATRICE MWAIPAJA NA PAUL CLEMENT WATASHIRIKI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam kuhusiana na  maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 litakalofanyika kwenye uwanja wa  CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2, 2018 Uwanja wa Halmashauri  mjini Bariadi mkoani Simiyu. Pembeni yake ni Mwimbaji Beatrice Mwaipaja na Mwimbaji Paul Clement.

Hayawi Hayawi sasa maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018, Kanda ya Ziwa katika jiji la Mwanza na Simiyu yamenoga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ameanza kutangaza waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo ambalo limekuwa likiwavutia waimbaji wengi kila linapoanza kuandaliwa na hatimaye kukamilika, Msama amemtaja mwimbaji mahiri jukwaani Boniface  Mwaiteje, Christina Shusho, Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake mpya siku hiyo, na wengineo ambao wanaendelea kujiunga kuhakikisha tamasha  hilo linafana. Pichani kulia ni mwimbaji Paul Clement pamoja na Beatrice Mwaipaja, ambao walitambulishwa rasmi hapo jana.

Mwimbaji Beatrice Mwaipaja akifafanua zaidi namna ambayo anaendelea kujiandaa na maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka 2018, Kanda ya Ziwa. Pembeni yake ni Mwimbaji Paul Clement.

Mwimbaji Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka 2018, Kanda ya Ziwa. Pembeni yake ni Mwimbaji Beatrice Mwaipaja.

No comments: