Friday, March 2, 2018

ANGALIA HAPA KUPATA RATIBA KAMILI YA MECHI ZA KESHO KWENYE LIGI KUU TANZANIA BARA MZUNGUKO WA 20

Mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara unaendelea kesho Jumamosi Machi 3,2018 kwa kuchezwa mechi nne.
        Tokeo la picha la ligi ya vodacom tz
Njombe Mji watakuwa nyumbani Uwanja wa Sabasaba kucheza na Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Kagare Sugar wao watakuwa nyumbani Uwanja wa Kaitaba kuwakaribisha Majimaji ya Songea mchezo utakaochezwa saa 10 jioni.

Mechi nyingine Tanzania Prisons ya Mbeya watakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza saa 10 jioni,Azam FC watakuwa Azam Complex ikiwakaribisha Singida United saa 1 jioni.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

No comments: