Sunday, March 4, 2018

MNEC SALIM ASAS AMPONGEZA MBUNGE ROSE TWEVE KWA KUINUA UCHUMI WA WANAWAKE WA WILAYA YA MUFINDI.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve akiongea mbele ya baraza kwa kuonyesha furaha yake mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas baada ya kuambiwa kuwa ataongezewa shilingi milioni kumi na nane kwa ajili ya maendeleo ya akina wanawake wa wilaya ya Mufindi
viongozi mbalimbali na wabunge wa viti maalum walihudhuria baraza hilo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Akingumza wakati wa baraza la UWT wilaya ya Mufindi Salim Asas alisema kuwa amefurahishwa na mkakati mbunge Rose Tweve kwa kufanikiwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kabisa ambao ndio wanastahili kuinuliwa kiuchumi kuliko wananchi ambao tayari wanauchumi mkubwa.

“Kwa kweli niwe muwazi kuwa nimefurahishwa na hiki kitu ambacho huyu mbunge anakifanya kwa kuwawezesha wananchi ambao ndio serikali ya awamu ya tano inataka kuwafikia na kuwainua kiuchumi” alisema Asas

Asas aliwata wabunge wengine kuiga mfano wa mbunge Tweve kwa kazi anayoifanya ya kuwawezesha akina mama na wananchi wengi kwa kuwa hiyo ndio inakuwa faida kwa taifa.
“Naombeni wabunge wangu wote tufanye kazi kama anayoifanya mbunge Rose Tweve kwa kuwafikia wananchi wa chini ambao mara nyingi imekuwa vigumu kuwafikia kutokana na sababu mbalimbali” alisema Asas

Aidha Asas alisema kutokana kazi kubwaanayoifanya mbunge Rose Tweve atachangia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi ambapo atatoa kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kwa ajili ya kuchangia vikundi hivyo.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.

Kaleghela alisema hadi kufika sasa mtaji umekuwa hadi kufikia shilingi milioni hamsini na mbili laki tano (52,500,000) na fedha hizo zinasimamiwa na umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi (UWT)

Bila mchango wa mbunge Rose Tweve tusingeweza kuwafikia wananchi kwa kiasi hiki hivyo nachukua nafasi hii pia kumpongeza mbunge wetu kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake mbunge Rose Tweve alikuwa ni mtu mwenye furaha baada ya kupokea hongera na kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kutoka kwa MNEC.

“Mnaniona nabubujika machozi kutokana na furaha niliyonayo kutoka na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas kutambua mchango wangu” alisema Tweve

No comments: