Kituo cha
radio cha Efm chenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam mapema leo
kimekutana na waandishi wa habari lengo likiwa ni
kujadili mambo makubwa
mawili.
Magari ya washindi wa mwaka jana wa shindano la shika ndinga mwaka 2017. |
Akiongea
katika mkutano huu Meneja Mkuu wa Efm radio na Tv E Bw. Dennis Busulwa alisema kuwa
lengo kuu la mkutano huo ni kuufahamisha uma kuwa mpaka kufikia tarehe 2 ya
mwezi 4 mwaka huu kituo hicho kinatimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake.
Aliongeza
kuwa mbali na sherehe hizo za kutimiza miaka minne lakini pia wako katika
mpango kabambe wa kulitangaza shindano lao la shika ndinga mwaka 2018
lotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Aidha meneja
Busulwa alisema kuwa katika sherehe hizo za miaka minne ya kituo hicho wataweza
kuongeza masafa yao katika mikoa mingine minne ambayo ni Dodoma, Morogoro,
Tabora na Kigoma.
Meneja huyo wa Efm alisisitiza kuwa mpaka sasa kituo chao cha matangazo kimekuwa cha kwanza kusikilizwa ndani ya mkoa wa Dar es salaam kwa utafiti uliyofanywa na mashirika binafsi na ni cha pili kusikilizwa kwa maeneo ambayo matangazo yao yanafika.
Ikimbukwe
kuwa mpaka sasa Efm inasikika katika mikoa sita ambayo ni Dar es salaam, Pwani,
Mbeya, Mtwara,Tanga na Mwanza na mpaka
kufikia siku hiyo ikiwashwa na hiyo minne itakuwa inasikika katika mikoa kumi
ndani ya Tanzania.
Kwa upande
wa shika ndinga 2018 safari hii mikoa itaongezeka siyo kama ilivyozoeleka kuwa
washiriki wanatoka Dar es salaam na Pwani peke yake.
“Kwa mwaka
huu wa 2018 shika ndinga itafanyika katika mikoa sita ambayo ni Dar es salaam,
Mtwara, Mbeya, Tanga, mwanza na Pwani na kila mkoa zitaweza kutolewa pikipiki
mbili na washiriki wa mikoani watagharamiwa na nauli kuja kushiriki fainali
itakayofanyika jijini Dar es salaam” alisema Meneje Busulwa
”Katika haya
mashindano ya mwaka huu yataweza kuwa na ubunifu tutaweza kumpata mshindi mmoja wa kiume na
mmoja wa kike ambao watapewa zawadi ya virikuu kila mmoja, lakini pia washindi wa
pili watapewa boda boda kila mmoja hii ikiwa ni njia yetu ya kuwawezesha
wasikilizaji wetu katika Nyanja ya uchumi” aliongezea Meneja Busulwa
Na wadhamini
wakubwa wa shika ndinga mwaka 2018 ni Shirika la simu la TTCL, Tatu Mzuka na Chotec wasambazaji wa
vilainishi vya shell Advance lakini pia watu watakao shiriki pamoja katika
kuadhimisha miaka minne ya Efm radio pamoja na TVE.
Meneja Mkuu wa Efm Radio pamoja na Tv E Bw. Dennis Busolwa akitoa maelezo mafupi kuhusu shidano la Shika Ndinga 2018 pamoja na miaka minne ya Efm Radio. |
No comments:
Post a Comment