Profesa Mwesiga Baregu asisitiza mambo makuu matatu muhimu kuwepo kwenye katiba mpya ili tunapoingia kwenye chaguzi zote mbili yasilete shida, ikiwemo uchaguzi mdogo wa mwaka 2019 na uchaguzi mkubwa wa mwaka 2020 mambo haya ni muhimu kuzingatiwa ili nchi isiingie kwenye machafuko
Muadhiri wa muda mrefu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye pia Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Profesa Mwesiga Baregu amesema bila kuwa na Katiba mpya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 basi taifa linaweza likapata matatizo.
Muadhiri wa muda mrefu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye pia Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Profesa Mwesiga Baregu amesema bila kuwa na Katiba mpya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 basi taifa linaweza likapata matatizo.
Amesema Dalili zipo wazi za nchi kuingia kwenye migongangono.
"Tumeshudia uchaguzi wa juzi Kinondoni jinsi mambo yalivyotokea,tusitake nchi ifike huku,sasa ni wajibu wa kuwa na Katiba mpya kuelekea kwenye uchaguzi wa 2020 ili nchi ivuke salama."amesema
Aidha Prof. Baregu alisema kuwa miongoni mwa mapendekezo ni kuwa na Tume huru ya Uchaguzi ili kuwa na matokeo yenye kusadikika na ya kweli na siyo tume zilizopo sasa ambazo zinapanga matokeo na kuchagua nani ashinde.
Aliendelea kusema kuwa jambo lingine lakufanyiwa marekebisho ni kuwa na mgombea huru katika chaguzi ili endapo mtu atahitaji kugombea aina haja mpaka awe na chama ndipo aweze kupewa nafasi katika chaguzi.
Katika mazungumzo hayo Prof. Baregu aliendelea kusisitiza swala la matokeo ya Urais kupingwa endapo itaonekana kama kuna vitu haviendi sawa kama illivyo katika katiba ya nchini Kenya hivyo hivyo iwe kwetu na endapo chama kimoja kitacheza mchezo mchafu kichukuliwe hatua na matokeo yake yasitambulike.
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ALIYOSEMA PROFESA...
No comments:
Post a Comment