Friday, March 2, 2018

ZOA ZOA YA CCM YAWAZOA VIONGOZI WAKUBWA KIBAO ACT WAZALENDO SOMA HAPA KUJUA

Wimbi la viongozi wa vyama vya upinzania kuviama vyama vyao na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) kimeendelea leo ambapo viongozi 12 kwa ngazi ya taifa mkoa, majimbo, na kata wa chama cha ACT-Wazalendo wamejiunga na CCM.
Tokeo la picha la act wazalendo
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam viongozi hao wamesema wamechukua jukumu hilo kutokana na kiongozi mkuu wa chama hicho zitto zubery kabwe kutoa matamko yaliyokinyume na misingi na kanuni ya chama hicho.

Viongozi waliojiuzulu na kujiunga na CCM ni Makamu mwenyekiti taifa zanzibar Ramadhan Ramadhan, Naibu katibu mkuu bara Leopold Lucas Mahona, Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Hudson Mwakyambiki, katibu wa chama mkoa wa Dar es salaam Ernest Kalumuna. 

Wengine ni katibu wa jimbo la ubungo Mikdadi Kirungi, katibu wa jimbo la kibamba Khalfan Sidadi, katibu mwenezi jimbo la ubungo Sadick Msangi, mwenyekiti wa ngome ya wanawake jimbo la ubungo Swaumu Msipu mwenyekiti ngowe ya vijana jimbo la ubungo Robert Kihiri mwenyekiti wa kata ya manzese Mtangi Semwanza na katibu wa chama kata ya manzese Ally Semwanza.

No comments: