Thursday, March 8, 2018

Uber ya sherekea wanawake wanaoendesha na Uber (International Women's Day 2018)

Kila siku ninafungua programu yangu ya Uber saa 12 asubuhi na ninaweza kufanya kazi hadi usiku. Katika kazi yangu ya udereva hakuna msafiri ambaye amewahi kunikosea heshima, sambamba na hilo sina cha kuogopa ninapotumia programu ya Uber.
Uber imeniwezesha kwa njia mbalimbali, ninaweza kufanya kazi muda ninaotaka na bado nitapata pesa za kutosha kuendesha maisha yangu ya kila siku. Imekuwa ni fursa yenye tija kubwa kwangu.
Glory Shirima
Mwanzoni haikuwa rahisi kuamini kwamba mwanamke anaweza kufanya kazi kama hii, kumchukua msafiri yeyote haikuwa jambo la rahisi. Lakini unapotumia Uber mambo ni tofauti kabisa, kwa sababu safari zangu zote zinawekewa kumbukumbu ninapata ujasiri kwamba kila kitu ni salama.
Nimekuwa nikitumia mfumo huu kwa kipindi kirefu, na ni matarajio yangu kwamba nitaendelea kutumia Uber kwa sababu ni njia mpya ya kujiajiri.

Khadija Sway
Uber imekuwa neema kubwa kwa sababu inarahisisha maisha ya madereva na wasafiri, mfumo mzima wa nauli ni nafuu sana kiasi kwamba watu wengi hawapati ugumu kulipia safari zao, sambamba na kupata safari nyingi iwezekanavyo.
Binafsi nimefurahi kupata fursa ya kupata kipato ambayo haina masharti magumu, najisikia nimewezeshwa kwa namna ya pekee kabisa. Gari langu ambalo ningelipaki nyumbani bila shughuli maalum sasa linaniletea kipato, limenisadia kujiari. Uber imenipa fursa ya kutumia gari langu kwa njia ambayo napata kipato cha kuendeshea maisha yangu.

No comments: