Leo ikiwa ni tarehe 8 ya mwezi machi nchi zote duniani zinasherekea siku ya mwanamke duniani kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni kuenzi na kupongeza michango mbalimbali iliyotolewa ama inayoendelea kutolewa na wanawake.
Mkurugenzi mtendaji wa Lecri Consult Bi. Edna Kamaleki akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kwa wageni waalikwa, katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani mapema leo jijini Dar es salaam. |
Katika kuhakikisha siku hii inaenziwa vyema mashirika mawili yaliyoamau kuungana na kufanya kitu kizuri kwa siku hii nayo ni Lecri Consult pamoja na Hodari Tanzania.
Na kwa mujibu wa kauli mbiu ya kimataifa ya mwaka huu inayosema “Chagiza maendeleo yako” hii ikijaribu kuwapa msukumo wanawake katika kujitafutia maendeleo yao wenyewe.
Mashirika hayo yameenzi siku hii kwa kufanya kongamano na wanawake pamoja na wanaume ili kuwajuza mambo mbalimbali ikiwa ni haki na wajibu wao kama wanawake na pia kuwapa mwanga wanaume nini cha kufanya ili kupunguza vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.
Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es salaam liliudhuliwa na maafisa mbalimbali kutoka serikalini na asasi za kiraia ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuelimishana mengi kuhusu haki zao kama wanawake.
Lakini pia katika kongamano hilo waliweza kuwaonyesha kwa kiasi gani wanawake wanaweza kuwa wamiliki wa ardhi yao wenyewe kwa mujibu wa sharia na sio kila siku kuwa nyuma ya mwamvuli wa wanume.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hodari Tanzania Bi. Emelda Lulu Urio akiendelea kutoa elimu kwa wanawake na wanaume waliofika katika tafrija hiyo. |
Mkurugenzi wa LAP kanda ya Dar es salaam Bi. Amina Kassim akiongea na wageni waalikwa. |
Mkurugenzi wa Benki ya NMB tawi la Samora Bw. Sospeter Magesse akielezea kwa namna gani benki hiyo inafanya kazi kwa ukaribu kwa kushirikiana na wanawake kote nchini. |
Maafisa kutoka mashirika mbalimbali ya kiserikali na binafsi wakifuatilia kwa umakini mawasilisho yanayotolewa na wawezeshaji. |
Washiriki wa maadhimisho wakiwa katika picha ya pamoja. |
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI YALIYOTOKEA..
No comments:
Post a Comment