MUIGIZAJi wa Bongo Movies, Irene Uwoya amesema anashangaa tangu aolewe na Dogo Janja, mwishoni mwa mwaka jana, wanaume wengi wamezidi kumtongoza siku hadi siku wakidhani anapatikana kirahisi.
Uwoya amesema kabla hajaolewa na Dogo Janja alikuwa hapati usumbufu kama huo lakini kwa sasa imekuwa too much.
Msanii huyo amedai kwamba Mama yake hakuhudhuria kwenye harusi yao kwa sababu alikuwa safarini mara kwa mara lakini kauli hiyo inakinzana na kauli ya wazazi wake wote wawili ambao kwenye mahojiano walisema hawajawahi kutambulishwa kwa huyo Dogo Janja.
Walidai mtoto wao, Uwoya hajawahi kumuambia mama hata baba yake kuhusu ndoa hiyo wala kuwajulisha kama ameolewa na Dogo Janja. .
Kauli ambayo imewafanya baadhi ya watu kuendelea kuamini kuwa Uwoya na Dogo Janja hawakufunga ndoa kweli ikiwa wazazi wake hawana taarifa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment