Watanzania wametakiwa
kuvifanya vitu vitatu muhimu katika maisha yao ya kila siku ili waweze kufikia
mafanikio moja ya vitu hivyo ni kujituma, kuwa tabia ya kuweka akiba na kuwekeza kwa ajili ya maisha yao ya baadae.
Hayo yamesemwa
jana na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
alipokuwa akizindua kitabu cha “Breaking the Chains of Poverty” kilichoandaliwa
na kuandikwa na shirika la World Vision.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam ulioudhuliwa na
wadau kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi zenye kulinda na
kutetea maslahi ya wananchi, wanawake pamoja na haki na ustawi wa mtoto.
“Napenda
jinsi shirika hili la World Vision linavyofanya kazi kwa kujaribu kuwaleta
pamoja watu wa dini zote na kuwajengea uwezo katika kujitafutia kipato bila
kuangalia itikadi au dini zao” alisema Waziri Ummy
“Sisi kama
serikali tunafurahi kuona mashirika binafsi yanajaribu kuwakomboa wananchi wanyonge
kwa kuwapa elimu na namna ya kujikomboa katika maisha haya, kwani hii inakuwa
imetusaidia majukumu yetu sisi kama serikali na kumpa moyo Rais wetu mpendwa Magufuli
katika juhudi zake za kuhitaji kila mtu afanye kazi ili kuweza kuijenga nchi
yetu” aliongezea ummy mwalimu
Aidha waziri
ummy alisema kuwa amekisoma kitabu kwa haraka haraka lakini amegundua kuwa kina
malengo mazuri kwa jamii ya kitanzania na afrika kwa ujumla kwani kinawapa
mwanga vijana na watu wa lika zote kuweza kujitafutia maisha kwa njia ya
ujasiriamali bila kukwaza watu wengine.
Waziri huyo
aliendelea kusema amefurahishwa na shuhuda za watanzania wengi ambao
wamefanikiwa kwa kujengewa uwezo kupitia semina zilizoendeshwa na shirika hilo
la World Vision, na hii inaonyesha kwa kiasi gani shirika hili linaweza kuwa
nuru kwa watanzania kujikomboa dhidi ya umasikini.
Viongozi wa dini ya kiislam na wakristo wakiwa pamoja katika sherehe za uzinduzi wa kitabu cha "Breaking the Chains of Poverty" kilichoandikwa na shirika la World Vision. |
Meza kuu ikifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika sherehe hizo. |
Baadhi ya watu waliofanikiwa kupitia mradi wa World Vision kwa kupewa elimu na baadae kujiendeleza wenyewe katika shughuli za ujasiriamali wakitoa shuhuda zao mapema jana jijini Dar es salaam. |
Margaret Schuler mbaye ni Makamu wa Rais wa shirika la World Vision nchini Marekani akitoa salamu za nchini huko na mipango ya shirika hilo kwa sasa. |
Waziri wa Afya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy mwalimu akiongea na hadhara iliyofika katika uzinduzi wa kitabu hicho mapema jana jijini Dar es salaam. |
Meza kuu wakisaini vitabu baada ya uzinduzi tayari kwa kuvigawa kwa washiriki wa tafrija hiyo fupi iliyofanyika mapema jana Serena hotel jijini Dar es salaam |
ANGALIA VIDEO HII KUSIKIA MENGI ALIYOSEMA WAZIRI UMMY..
No comments:
Post a Comment