Serikali
imetakiwa kutoa taulo za kujihifadhia(Ped) bure kwa watoto wa kike katika shule za
msingi na sekondari, kwani hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wa kike
kukosa masomo kwa siku kadhaa.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Upendo Peneza akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika semina za Jinsia na Maendeleo(GDSS) mapema jana ofisi za TGNP Mtandao. |
Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mbunge wa viti Maalum kupitia CHADEMA Mh. Upendo Peneza alipokuwa akiwaelezea washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo(GDSS) jinsi alivyopeleka hoja hiyo bungeni.
Aidha Muheshimiwa
Upendo alisema kuwa ikiwa serikali imeweza kutoa elimu bure kwa watoto wote
kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari, hivyo haitashindwa kutoa pedi kwa
watoto hawa kwani hali hii inawaathiri watoto wengi wa kike kwa kukosa masomo
kwa siku 4 mpaka 5 ambazo ukijumlisha kwa mwaka ni siku nyingi sana hali
inayosababisha watoto wengi kutokuwa uwezo mzuri darasani.
Mbunge huyo
aliendelea kusema kuwa hoja hiyo haikuweza kupitishwa ndani ya Bunge ili kuweza
kujadiliwa kwa madai ya serikali kuwa amevunja sharia 99 kipengele cha 2 cha
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini baadae kamati ya huduma za jamii ya Bunge ilikubali na kuhitaji mapendekezo kwa wabunge kuweza kupitisha au kukataa.
“Licha ya
serikali kukubali hoja hiyo lakini mpaka leo haijatoa tamko lolote kuhusiana na
kutoa pedi hizo bure, lakini mimi kama kiongozi najaribu kuikumbusha serikali
kwa kuiandikia barua, kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika
kupaza sauti zetu kwa pamoja ili kusaidia jambo hili na pia kuirudisha hoja
hiyo tena bungeni kwa kuona kama inaweza kupewa kipaumbele katika bajeti ya
mwaka huu 2018/2019.” alisema Upendo
Mh. Upendo aliendelea
kusema kuwa tunapigania watoto wetu waweze kuapata taulo za kujihifadhia bure
ili kujenga taifa bora lenye usawa hivyo kwa mwaka huu wa fedha ikishindikana
kutengwa pesa kwa jambo hilo basi serikali iondoe hata kodi kwa vifaa hivyo ili
kupunguza mzigo kwa wazazi na jamii nzima kwa ujumla.
Mbunge huyo
aliongezea kwa kusema kuwa kwa ustawi na ukuaji mzuri wa watoto wa kike ni
kuwajengea mazingira mazuri kama kuongeza matundu ya vyoo kuwapatia taulo za
kujihifadhia wakiwa katika siku zao pamoja na vyumba ya kujihifadhia mashuleni.
Na mwisho
aliongezea kwa kusema kuwa pia hata katika taulo za kujihifadhia zipo za aina
mbili kuna za kufua zikichafuka na nyingine zikichafuka unatupa, lakini ni
nzuri za kutumia na kutupa kwani zile nyingine zinaweza kuleta maradhi endapo
zitakosa matunzo mazuri hali itakayosababisha serikali kutumia fedha nyingi
katika kuwapa matibabu watoto hao.
Mshiriki wa semina Betty Kazimbaya akichangia mada katika semina ya jinsia na maendeleo(GDSS) jana jijini dar es salaam |
ANGALIA VIDEO HII KUJUA MENGI ZAIDI..
No comments:
Post a Comment