Baada ya zaidi ya muongo mmoja na nusu kufikia Azaki nchi nzima, Sasa Foundation for
Civil Society (FCS) inajikita katika kuongeza ufanisi na juhudi za kufanya kazi
kwa ushirikiano na wadau wote katika kuleta maendeleo.
Hayo
yameelezwa mapema jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw.
Francis Kiwanga wakati wa uzinduzi nembo mpya ya shirika hilo ambayo itaendana
na mabadiliko na mfumo wake wa utendaji.
Alisema kuwa
hii itahusisha kushirikiana na taasisi zote za Serikali, Bunge, Sekta binafsi,
Asasi za kiraia (AZAKI) ili kufikia Maendeleo Endelevu ya Dunia pamoja na Mpango
wa Maendeleo wa Taifa wa kuboresha maisha ya watanzania ifikapo 2025.
Aidha
aliongeza kuwa kwa sasa FCS itatoa ruzuku kwa wastani wa Asasi 150 kwa pande
zote mbili za muungano yaani Tanzania Bara na Visiwani kila mwaka, ambapo hapo
awali ilikuwa ikitoa kwa Azaki zaidi ya 5500 zilizokuwa zikihudumia wananchi wa
mikoa yote hapa nchini.
Alisisitiza
kuwa kiasi cha ruzuku kitaongezeka na kwa sasa taasisi hiyo itatoa ruzuku zenye
thamani ya billion 11. kwa mwaka na muda wa mkataba pia utakuwa mrefu hadi
kufikia miaka miwili ili kupata matokeo mazuri kwa miradi itakayofadhiliwa na FCS.
Akieleza sababu
ya kufanya hivyo alisema kuwa wamejikita katika eneo la utawala bora na
maendeleo hivyo siyo rahisi kuboresha maeneo hayo kwa mkataba wa mwaka mmoja au
miezi sita tu, Hivyo wameona kuna haja ya kuongeza mkataba na kiwango cha
ruzuku katika kufanikisha hili.
Na mwisho
kabisa alipenda watu wafahamu kuwa FCS ipo kwa ajili ya watanzania hivyo
waondoe mila potofu ya kuwa ni chombo ambacho hakina ubia na serikali na kwa
sasa watafanya mambo mengi mazuri kwa kushirikiana na serikali katika kuleta
maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.
Mazungumzo ya azaki yanaendelea kupitia hastag hizi.
#AZAKITanzania / #CivilSocietyTanzania
Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Foundation for Civil Society likifanyika.
Mazungumzo ya azaki yanaendelea kupitia hastag hizi.
#AZAKITanzania / #CivilSocietyTanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis kiwanga akitoa maana ya kitu kimoja baaba ya kimoja katika nembo ya kwanza ya shirika hilo kabla ya kuzinduliwa kwa nembo mpya.
Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Foundation for Civil Society likifanyika.
Baadhi ya washiriki kutoka AZAKI mbalimbali hapa nchini wakifuatilia matukio yanayoendelea katika Tafrija hiyo ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS.
Baada ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS kulifuatiwa na tukio lingine la uzinduzi wa tovuti mpya (Website) mpya ya shirika hilo kama inavyoonekana pichani.
Washiriki wa semina wakiendelea kusherehekea tafrija.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa shirika la Foundation For Civil Society.
Wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tafrija hiyo, Ambao pia ni wana AZAKI wanaofanyanao kazi kupitia miladi mbalimbali wanayoiendesha.
No comments:
Post a Comment