Ufanisi katika jambo lolote lenye tija na manufaa ni kitu muhimu sana na sasa huduma ya usafiri wa kukodi unaotolewa na Uber imefungua ukurasa mpya kwa kuamua kufanya kazi na Tigo Tanzania.
Usafiri wa kukodi, Uber umekuwa na umaarufu wake kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam na hivyo kuwa na mvuto kwa wengi hasa wale ambao hawapendi kupata shida ya kugombania usafiri au kufika sehemu ambayo mtu anakwenda bila nguo yake kuchafuka kwa vumbi/majasho.
Unaweza ukajiuliza nini ambacho kimewaleta Uber na Tigo katika meza moja na kuamua kufanya kazi kwa pamoja? Jibu ni rahisi sana, teknolojia lakini utauliza tena kivipi? Uber anamiliki programu tumishi na ili uweze kuita huduma ya usafiri wa Uber basi itakubidi uwe na kifurushi cha intaneti (MBs).Watumiaji wote wa app ya Uber na wanaotumia laini ya Tigo hawatatozwa kiasi chochote cha kifurushi cha intaneti wanapokuwa wanatumia programu tumishi ya Uber.
Uwezo wa kutumia app ya Uber bila kifurushi chako cha intaneti kutumika ni kwa wote, dereva pamoja na abiria anayetumia laini ya TIgo.
No comments:
Post a Comment