Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga akiwa pamoja wasanii wa Bongo Flava Joh Makini na Mimi Mars alipotangaza punguzo kubwa la bei za tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na zawadi za hadi TSH 50 millioni kupitia promosheni ya Jigiftishe kuelekea kilele cha tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Katibu Kiongozi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner Habash (kati) akiwa pamoja na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga na msanii wa Bongo Flava, Fareed Kubanda – Fid Q (kulia) walipotangaza kuwa wateja wote watakaotumia usafiri wa Uber Jumamosi hii kwenda kushuhudia kilele cha tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama lote katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam watapokea punguzo la TSH 5,000 kwa usafiri huo.
Msanii wa Bongo Flava, Mimi Mars akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandilizi ya kilele cha tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote litakalofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tigo imetangaza punguzo kubwa la bei kwa tiketi zote zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Msanii wa Bongo Flava Whozu (wa tatu kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadalizi ya kilele cha tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote litakalofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) alitangaza ofa kabambe kutoka Tigo ikiwemo punguzo kubwa la bei kwa tiketi zote zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga pamoja na Katibu Kiongozi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner Habash (kati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika kilele cha msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote siku ya Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Haya ndio magari ya Uber ambayo yatawabeba watu kwa bei nafuu kabisa kuelekea katika viwanja vya leaders kupata Burudani ya nguvu ya Tamasha kubwa la
Tigo Fiesta 2018 Vibe kama lote
(Picha kwa msaada wa Mwanaharakati Mzalendo)
Tigo Fiesta 2018 Vibe kama lote
(Picha kwa msaada wa Mwanaharakati Mzalendo)
- Mashabiki kufurahia punguzo kubwa la bei za tiketi na zawadi za fedha taslimu
- Tigo, Uber waungana kutoa usafiri salama, wa uhakika kwa gharama nafuu
Dar es Salaam, Novemba 22, 2018 – Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikianiana na kampuni ya Clouds Media Group, imejiandaa vilivyo kuwapa burudani ya kufunga mwaka wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani kupitia Tamasha kubwa la Tigo Fieast 2018 Vibe Kama Lote litakalofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.
Mashabiki wa muziki watafurahia punguzo kubwa la bei kwa tiketi za kuingia katika tamasha hilo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati watakaponunua tiketi kwa Tigo Pesa/Masterpass QR.
‘Tigo inatoa punguzo kubwa la zaidi ya asilimia 30% kwa tiketi za tamasha la Dar es Salaam zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa/Masterpass QR. Tiketi za tamasha hilo zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 10,000 kupitia Tigo Pesa/Masterpass QR badala ya bei ya TSH 15,000 itakayotumika kwa tiketi zitakazonunuliwa mlangoni,’ Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
Ili kupata ofa hiyo ya tiketi, wateja wa Tigo wanapaswa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), kubonyeza 2 (lipa Masterpass QR) na kisha kutuma gharama husika ya TSH 10,000 pekee kwenda kwa namba ya Tigo Fiesta 78888888. Ofa hii pia ipo wazi kwa watumiaji wa mitandao mingine wanaopaswa kufuata hatua za kawaida wanazotumia kutuma pesa katika mitandao husika.
‘Kila wanaponunua tiketi kwa njia ya Masterpass QR, wateja wa Tigo pia wanajiongezea nafasi ya kushinda TSH 1 milioni kila siku, TSH 10 milioni kila wiki ama hadi TSH 50 milioni katika promosheni kubwa ya Jigiftishe inayotoa zawadi za pesa taslim katika msimu huu Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya,’” William aliongeza. Promosheni hiyo kabambe ya Jigiftishe inawazawadia wateja kwa kutumia huduma za Tigo, bila masharti yoyote wala ulazima wa kujiunga na promosheni yenyewe.
Wateja wote wa Tigo pia wana fursa ya kushinda donge nono la TSH 100,000 kila siku, TSH milioni moja kila wiki au hadi TSH 10 milioni katika droo kubwa ya shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo Trivia. Kujiunga na shindano hilo linalopima ufahamu wa washiriki kuhusu masuala ya muziki na burudani, mteja anapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda namba 15571 ama kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kisha kuchagua Trivia.
Kwa kutambua kuwa usafiri wa uhakika ni mojawapo ya changamoto kwa mashabiki watakaohudhuria tamasha la Tigo Fiesta, kampuni ya Tigo pia imeingia katika makubaliano na kampuni ya teknologia ya Uber ili kurahisisha suala la usafiri.
‘Jumamosi hii, Tigo na Uber wanatoa punguzo kubwa la TSH 5,000 kwa mashabiki wote watakaotumia usafiri wa Uber kwenda na kutoka kuhudhuria tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote katika viwanja vya Leaders. Kwa kutumia Uber App kwenda na kutoka kwenye tamasha hilo, maelfu ya wapenzi wa muziki watafurahia faida za usafiri wa uhakika, rahisi, salama na kwa gharama nafuu,” William alisema.
Baada ya kuzuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linahitimisha mwaka wake wa 17 huku likiwa limetimiza ahadi yake ya kukuza viwango vya muziki wa nyumbani na kukuza wasanii wa ndani ili wafikie viwango vya kimataifa.
Wafanyabiashara pamoja na viongozi wa serikali katika mikoa yote iliyoshuhudia tamasha hilo mwaka huu wamepongeza mchango mkubwa wa Tigo Fiesta 2018 katika kuibua fursa za biashara katika maeneo husika. Wafanyabishara waliofaidi zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaohudhuria tamasha hilo ni pamoja na wamiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni, migahawa na mama nitilie, wenye maduka, wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki wa vyombo vya usafiri kama daladala na bodaboda pamoja na watoaji wa huduma nyingine mbalimbali. Fursa nyingi zaidi za biashara zinatarajiwa kuibuliwa katika tamasha la kufunga msimu jijjni Dar es Salaam litakaloanza saa kumi na mbili jioni hadi majogooo.
Waandaaji Clouds Media Group kupitia Katibu Mkuu Kiongozi wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash wamebainisha kuwa tamasha la kufunga msimu litashuhudia wasanii wanaochipuka kutoka mikoa 14 ya nchi wanaoshiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 Supa Nyota wakipanda jukwaani kutuo burudani kuwasindikiza wasanii wakongwe wa bongo flava. “Kufikia sasa tuna wasanii zaidi ya 30 watakaotumbuiza katika tamasha la Dar es Salaam na tunazidi kusajili wasanii wengine kwa hiyo wapenzi wa muziki wajiandae kupata shoo kali na vibes za uhakika Jumamosi hii,’ Gardner alisema.
No comments:
Post a Comment